Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Saturday, 25 April 2015

SIKU YA MALARIA DUNIANI: WATAKAOTUMIA VYANDARUA KINYUME NA MATUMIZI YAKE KUKIONA CHAMOTO, NI WALE WANAOFUGIA KUKU, KUVULIA SAMAKI NA KUFANYIA SHUGHULI ZA KILIMO
Tanzania leo imeungana na dunia yote kwa kuadhimisha siku ya Malaria duniani, maadhimisho ambayo huadhimishwa kila Aprili 25 ambapo kitaifa yamefanyika jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mnazi mmoja na kuongozwa na Mkuu wa Mkoa Mhe Said Meck Sadick.


Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amesema kwamba ifike wakati kila mwananchi atambue madhara ya ugonjwa wa Malaria na kuchukua hatua stahiki mara anapohisi dalili za ugonjwa huo kwa kufika mapema katka vituo vya afya.

Aidha, Sadick amewataka wananchi kuachana na tabia ya kumeza dawa bila kupima, huku akisema kuwa si 'kila homa ni Malaria' hivyo ni lazima kupima kabla ya kuanza kumeza dawa za Malaria.

“Lazima upime na dokta adhibitishe kwanza kama Malaria imo ili aweze kukupatia dozi inayofanana na malaria iliyopo katika damu” alisema Sadick.

Pia, Sadick alibainisha kwamba juhudi za serikali na sekta binafsi pamoja na wadau mbalimbali kwa kiasi kikubwa zimechangia kupunguza vifo vitokanavyo na ugonjwa huo kutoka asilia 18 mwaka 2008 hadi asilimia 10 mwaka 2012.

Kutokana na hali hiyo amesema imechangia kwa kiasi kikubwa kumbunguza vifo vya kinamama wajawazito na watoto wenye umri wa miaka chini ya mitano ambao ndio wamekuwa wakipoteza maisha zaidi kutokana na Malaria.

Pamoja na hayo, Sadick amesema serikali ipo katika mpango mkakati wa kuzindua rasmi zoezi la ugawaji wa vyandarua kila kaya nchi nzima, ambapo kila chandarua kimoja kitagawiwa kwa watu wawili, hivyo katika zoezi hilo Serikali inataraji kutoa vyandarua milioni ishirini na mbili.

Hali kadhalika, amewasisitiza wananchi kuzingatia matumizi ya vyandarua hivyo na kuachana na tabia ya kuvulia samaki , kufugia kuku au kufunikia mboga (bustanini) ili zisiliwe na wadudu na kusema kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na atakayebainika atachukuliwa hatua kali na serikali.

“Tunaomba viongozi wa serikali za mitaa na vijiji kwa yoyote atakayekiuka matumizi ya vyandarua hivyo achukuliwe hatua, kwahiyo nawataka viongozi wote wafuatilie kwa ukaribu matumizi ya vyandarua.” alisema Sadick

Mbali na hayo, Sadick amewataka Watanzani kupambana kwa dhati na ugonjwa wa malaria na kutambua kuwa ugonjwa huo ni chanzo cha umasikini miongoni mwa jamii, huku akizitaka taasisi za kuhakiki viwango nchini zikiwemo TFDA na TBS kuendelea kushirikiana katika kuhakikisha madawa yanayokuja nchini yanakuwa na ubora unaotakiwa.

Miongoni mwa mikakati ambayo imepewa kipaumbele katika kupambana na ugonjwa huu ni pamoja na udhibiti wa mbu waenezao malaria kwa kutumia vyandarua vyenye viuatilifu na kuharibu mazalia ya mbu, utoaji wa tiba sahihi ya malaria pamoja na kuhakikisha elimu inawafikia zaidi wananchi juu ya ugonjwa huo.

Karibu Mandai Herbal Clinic, tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment