Saturday, 11 April 2015

TAFITI: MWANAUME MMOJA KATI YA KUMI HUPIGWA NA WAKE ZAO
IMEELEZWA kwamba mwanaume mmoja kati ya wanaume 10 wa nchini Kenya hupigwa na wake zao ama wapenzi wao.


Kwa mujibu wa utafiti wa kiafya uliofanywa nchini humo umeonesha kwamba wanaume walio kati ya umri wa miaka 20 hadi 24, ambao ni asilimia 11.7 wamekuwa wakivumilia unyanyasaji huo, huku wakifuatiwa kwa karibu na wale walio na umri kati ya miaka 40 na 49 ikiwa ni asilimia 9.8.

Aidha, wale walio kati ya miaka 30 na 39 waliripoti visa vichache, huku asilimia 7.1 wakisema kuwa walinyanyaswa kulingana na utafiti huo wa mwaka 2014.

Utafiti huo uliainisha kuwa, wanaume waliopewa talaka ama hata kutengana na wake zao walilipoti visa vya juu vya unyanyasaji.

Mbali na hayo, ni asilimia 7.1 ya wanaume ambao wanaishi na wake zao ambao wameripoti visa vya kupigwa.

Pamoja na hayo, wanaume ambao hawakukamirisha elimu ya msingi waliripoti visa vingi vya unyanyasaji wakifuatiwa na wale ambao wamekamirisha masomo ya msingi na yale ya shule za upili.

Unaweza kufika Mandai Herbal Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam kama unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali. Au wasilina na Dk Mandai kwa mawasiliano yafuatayo: 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com 

No comments:

Post a Comment