Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 18 April 2015

TAFITI: WANAUME WANAONGOZA KWA MATUKIO YA KUJIUA KULIKO WANAWAKE




Imeelezwa kuwa wanaume wengi wenye umri kati ya miaka arobaini na 50 wapo katika hatari kubwa ya kujiua kuliko wanawake.


Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na kijana mmoja kutoka nchini Uingereza, Simon Jack alifanya utafiti huo baada ya baba yake kujiua katika siku yake ya kuzaliwa miaka 25 iliyopita akiwa na umri wa miaka 44.

Kijana huyo anasema alianza kuwa mdadisi kwa simulizi zote au habari kuhusu watu wanaojiua na amegundua kuwa wote ni wanaume.

“Wanaume wanazongwa na mawazo na hawana wa kusema naye” alisema Jack.

Aidha, Jack aliongeza kuwa ''sikujua kuwa kujiua ni adui mkubwa wa watu wenye umri chini ya miaka 50, ila sasa nafahamu kwanini wanaume mia moja wamejiua ndani ya wiki''.

Idadi hiyo imekuwa kubwa zaidi kuliko wakati wowote katika miaka 14 iliyopita ya wanaume wanaomaliza maisha yao wenyewe ni mara nne ya wanawake.

Jack, anasema kwamba alitamani kufahamu sababu inayowafanya wanaume kufanya matukio hayo zaidi na kama kuna namna yeyote ya kuzuia mauaji hayo.

Simon Jack akielezea matokeo ya utafiti wake huo alisema ''miaka 40 ni miaka ambayo mtu ana majukumu mengi, unaweza kudhani kuwa mke wake amemuacha na kuchukua watoto wote au kapoteza kazi yake katika umri huo wakati ni vigumu kupata mwingine'' alihoji Jack.

Aliendelea kusema kuwa ''au sababu yoyote ambayo inaweza kumpa shinikizo mwanaume ambaye anahitajika kuhudumia familia yake''.

Kwa upande wa baba yake Jack, haikuwa hivyo kwani alikuwa ni baba mzuri mwenye upendo kwa familia yake, mwenye uwezo na umaarufu.

Kila mtu atakubali kuwa ni tatizo kubwa katika familia pale unapompoteza mtu kwa sababu ya ugumu wa maisha uliokithiri au kuachwa na mpendwa wako.

Katika utafiti huo pia wengine walitoa maoni kuwa wengi wanaojiua ni ushahidi tosha kuwa wana matatizo ya kiakili au wana msongo wa mawazo au huzuni katika maisha.

Prof Rory O'Connor ambaye anaongoza kituo maarufu duniani cha utafiti katika Chuo Kikuu cha Glasgow, yeye anasema tabia ya kujiua ni tatizo la kisaikolojia ambalo hutokana na upungufu wa kiakili.

Hata hivyo, Jack anasema watu wenye matatizo ya akili huwa ni vigumu sana kujiua ni asilimia tano tu ndio wanaweza kujiua kutokana na upungufu wa akili.

Pia utafiti huo ulibaini kwamba katika maamuzi kuna tofauti kubwa kati ya namna wanaume na wanawake wanavyo weza kujielezea matatizo yao na kuyatatua.

''wanawake huwa wanatumia njia za kujieleza ambazo ni rahisi watu kumuokoa tofauti na wanaume''

Mbali na hayo, Jack anasema “natamani kujua nini kilimpata baba yangu kwani fumbo hili linaweza jibu maswali ya familia nyingi wenye matatizo kama yangu”.

No comments:

Post a Comment