Thursday, 16 April 2015

TATIZO LA UGUMBA HUWATESA WANAWAKE, HAPA KUNASABABU ZAKEWanawake wengi wamekuwa wakisumbuliwa na matatizo ya uzazi hivyo nimeona leo ni bora tuelimishane kuhusiana na tatizo la ugumba.


Kwanza kabisa ifahamike kwamba ugumba kwa mwanamke ni ile hali ya kushindwa kupata ujauzito kwa mwanamke, lakini wakati huo huo akishindwa kupata ujauzito wakati anashiriki tendo la ndoa vizuri kwa muda mrefu takribani mwaka mmoja pasipo kutumia kinga yoyote. Kwa maana nyingine anashiriki akitarajia kupata mtoto.

Tatizo hili la ugumba limegawanyika katika sehemu mbili nazo ni ‘Primary Infertility’ ambayo hii ni ya mwanamke ambaye hana historia ya kupata ujauzito.

Sehemu ya pili ni ‘Secondary Infertility’ ambayo hii ni mwanamke anakuwa tayari huko nyuma alishawahi kupata ujauzito, haijalishi alizaa au mimba iliharibika.

Sababu za Mwanamke kuwa Mgumba..
Ovulatory
Kwanza kabisa ni chanzo kinachohusu upevushaji wa mayai (ovulatory). Hili ndilo tatizo la kwanza kabisa ambalo linawaathiri wanawake wengi kwa kiasi kikubwa, ambapo mwanamke anapata siku zake kama kawaida , lakini hapevushi  mayai. Hii husababishwa na matatizo ya homoni mwilini. Tatizo linaweza kutokea lenyewe kutokana na mabadiliko ya mwili.

Wingi au Uchache wa Homoni
Tatizo lingine ni wingi au uchache wa homoni ambazo huchangia kukosekana kwa mayai yaliyopevushwa kipindi Fulani na hupelekea mwanamke kushindwa kupata ujauzito.

Kuharibika kwa kizazi
Kuharibiwa kwa kizazi kwa namna moja au nyingine huweza kusababisha kuwa mgumba. Mfano kuna baadhi ya wanawake huathiriwa na bacteria ambao hawana madhara yoyote, lakini wanapoongezeka au kuzidi kutokana na matumizi ya' antibiotic' huathiri mfumo wa kizazi cha mwanamke.

Hizo ni baadhi ya sababu zinazoweza kuchangia ugumba kwa mwanamke, lakini endelea kutembelea tovuti hii nitakuletea sababu nyingine zaidi.

Karibu Mandai Herbal Clinic kama unasumbuliwa na magonjwa sugu au unahitaji ushauri juu ya masuala mbalimbali ya kiafya. Tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Au wasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kulike page yetu ya facebook iitwayo Mandai Herbalist Clinic-mhc ili ufikiwe na taarifa zetu kila siku

No comments:

Post a Comment