Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 27 April 2015

TUNDA LA PESHENI LIMESHEHENI VITAMINI NYINGI
Matunda ya mapesheni kwa jina la kitaalam linajulikana kama ‘passifl ora edulis’ ni zao lenye asili ya Marekani ya Kusini na inaaminika kuwa kwa mara ya kwanza mmea wa mpesheni ulipandwa nchini Hawaii ukitokea Australia mnamo mwaka 1880.


Mpesheni ni mmea unaokuwa kwa kutambaa, hivyo katika ukuaji wake ni muhimu kuweka miti ili iweze kusaidia kutambaa juu yake.

Kwa hapa nchini kwetu (Tanzania) zao hili hulimwa sana katika maeneo ya Zanzibar, Morogoro, Dar es Salaam, Kigoma, Kilimanjaro, Tanga, Arusha pamoja na mkoa wa Pwani.

Mapesheni yanasifika kwa kuwa na virutubisho bora kwa afya ya binadamu ikiwemo vitamin C, A, B2, B6, C, na E, flavonoids, pectin pamoja na madini ya chuma.

Mpesheni huweza kusaidia kupunguza maumivu ya mishipa ya fahamu na maumivu ya tumbo la hedhi, hali kadhalika husaidia kutibu matatizo ya wasiwasi, msongo wa mawazo na hali ya kuzubaa kwa wazee na watoto.

Hata hivyo, watafiti wanasema kuwa, wajawazito na watoto wachanga wanapaswa kuchukua tahadhari wanapotumia tunda hili, hii ni kutokana na katika majaribio ya utafiti huo walibaini matunda hayo yanauwezo wa kusababisha uchungu na kusababisha watoto kuzaliwa kabla ya wakati, lakini pia huweza kusababisha usingizi hivyo si vizuri kutumiwa na madereva.

KARIBU MANDAI HERBALIST CLINIC, UPATE TIBA SAHIHI NA MAKINI KWA KUTUMIA DAWA ASILI ZITOKANAZO NA MIMEA NA MATUNDA NA HAZINA KEMIKALI NA NI SALAMA KWA MATUMIZI YA BINADAMU. UNAWEZA KUWASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443 AU dkmandaitz@gmail.com. TUPO UKONGA, MONGOLANDEGE JIJINI DAR ES SALAAM.

No comments:

Post a Comment