Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 15 April 2015

UGONJWA WA KIFAFA
Kifafa ni ugonjwa unaosababishwa na hitilafu zinazotokea sehemu ya ubongo.

Pale mtu anapozirai kwa ghafla huathiri ubongo kufanya kazi na kusababisha mtu kupata mabadiliko ya ghafla katika fahamu, mwendo ama hisia.

Kuzirai mara moja kunaweza kutokea kwa sababu tofauti kama vile mtu kuwa na homa, jeraha la kichwa au kiwango cha chini cha sukari katika damu.

Lakini kifafa maana yake ni kuzirai kwa ghafla kunapotokea zaidi ya mara moja bila ya sababu.

 Mtu mwenye kifafa huweza kuzirai na kuanguka chini na kugaragara na huwa hawezi kujizuia  na huweza kurudiwa na  fahamu baada ya muda fulani.

Pia mtu mwenye kifafa huweza kupoteza udhibiti wa misuli yake na kuangusha kile alichokuwa amekishikilia, lakini wakati mwingine mhusika anapojaribu kutembea huweza kuanguka chini na asiweze kujizuia.

Hata hivyo ni vyema ikafahamika kwamba ugonjwa wa kifafa unaweza kumuathiri mtu yeyote katika umri wowote. Licha ya kwamba mara nyingi kifafa huanza utotoni na mara chache kwa watu wazima, lakini kama kitaanza kwa mtu mzima mara nyingi panakuwepo na visababishi vinavyojulikana.

Moja ya dalili ya mtu mwenye tatizo hili ni pamoja na pale mtu anapozirai mara ya kwanza na katika historia yake hajawai kuwa na kifafa, mtu huyu anahitaji kumuona daktari mara moja.

Visababishi vya tatizo.
·         Havijulikani
·        Ajali mbaya ya kichwa.
·        Kufeli kwa figo.
·        Matumizi mabaya ya dawa na pombe
·        Kaswende iliyosambaa kwenye mfumo wa fahamu.
·        Sukari kushuka kwenye damu.
·        Stroke

 Karibu Mandai Herbal Clinic kama unasumbuliwa na magonjwa sugu au unahitaji ushauri juu ya masuala mbalimbali ya kiafya. Tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Au wasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kulike page yetu ya facebook iitwayo Mandai Herbalist Clinic-mhc ili ufikiwe na taarifa zetu kila siku

No comments:

Post a Comment