Wednesday, 8 April 2015

UNENE KUPITA KIASI NI HATARI, SOMA HAPA NAMNA YA KUKABILIANA NA UNENE KUPITILIZAMara nyingi tumekuwa tukipokea maswali kutoka kwa wadau wetu wakihitaji kujua ni namna gani wanaweza kupunguza unene uliopitiliza.


Hivyo leo nimeona nikusogezee hizi njia kadhaa ambazo unaweza kuanza nazo katika kukusaidia kupunguza unene uliopitiliza.

1.     Jenga utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara

2.     Pendelea kula matunda kwa wingi pamoja na mbogamboga.

3.     Jenga utamaduni wa kula nafaka ambazo hazijakobolewa hususani unga wa dona


4.     Epuka matumizi ya kula vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi pamoja na kupunguza kula vyakula vya wanga kupita kiasi.

5.     Jenga utamaduni wa kutumia vyakula vyenye calcium kwa wingi

Pamoja na kukujuza njia hizo zinazoweza kukusaidia katika kupunguza unene kupita kiasi, lakini ni vyema ikafahamika kwamba kupunguza unene hakumaanishi kuwa mtu anatakiwa kupunguza kula isipokuwa jambo la msingi ni kuhakikisha unakula chakula bora.

Mbali na hayo, kuna mambo yanayochangia mtu kuwa mnene, lakini sababu kubwa ni mtindo wa maisha ikiwemo vyakula tunavyokula.

Miongoni mwa sababu zinazochangia unene kupita kaisi ni sambamba na ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi, kutofanya mazoezi, kula vyakula vyenye wanga pamoja na kurithi.

Inawezekana umekuwa ukisumbuliwa na magonjwa sugu kwa muda mrefu na hujajua ni wapi sehemu sahihi ya kuondokana na  magonjwa yanayokusumbua, Napenda kukupatia namba hizi za simu kutoka Mandai Herbal Clinic ili uwasiliane nasi sasa na hakika itakuwa mwanzo wa kumaliza shida ya ugonjwa unaokusumbua namba zetu ni 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Piga sasa uone mafanikio katika afya yako.  

No comments:

Post a Comment