Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 16 April 2015

UTAFITI:TALAKA ZINACHANGIA WATU KUPATA UGONJWA WA MOYOKama ulikuwa ukiwaza kutoa talaka kwa mwenzi wako ni vyema ukasitisha mpango huo kutokana na zoezi hilo kuelezwa kuwa huweza kuchangia mhusika kupata ugonjwa wa mshtuko wa moyo.


Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika nchini Marekani umeeleza kuwa watu walio katika talaka wana uwezekano mkubwa wa kupatwa na ugonjwa wa mshtuko wa moyo ukilinganisha na wale ambao bado wako katika ndoa.

Utafiti huo ulifanyika kwa watu 15,827 na umeonesha kuwa wanawake ndio walioathirika zaidi na kwamba hupunguza hatari hiyo baada ya kuolewa tena.

Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Journal unasema kuwa msongo wa mawazo kupitia kiasi unaohusishwa na talaka una athari za mda mrefu katika mwili.

Asilimia 24 ya wanawake wanaotalaki mara moja hukabiliwa na tishio la ugonjwa huo wa moyo ikilinganishwa na wanawake ambao wameolewa.

Takwimu hizo pia zinasema kuwa wale ambao wamekuwa na misururu ya talaka wako asilimia 77 kupatwa na ugonjwa huo.


Karibu Mandai Herbal Clinic kama unasumbuliwa na magonjwa sugu au unahitaji ushauri juu ya masuala mbalimbali ya kiafya. Tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Au wasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kulike page yetu ya facebook iitwayo Mandai Herbalist Clinic-mhc ili ufikiwe na taarifa zetu kila siku


No comments:

Post a Comment