Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 7 April 2015

VIFAHAMU VYAKULA UNAVYOPASWA KULA WAKATI WA KIPINDI CHA BARIDIWatu wengi huwa hawafahamu ni vyakula gani hufaa kuliwa kipindi cha wakati wa baridi hivyo leo hii nimekuwekea hapa baadhi ya vyakula hivyo.

Kabeji ni mojawapo ya mboga yenye umuhimu katika mlo, kutokana na kuwa na virutubisho vya kutosha, pia ni moja ya mboga yenye vitamin A na ndani yake ina madini ya  lutein na zeaxanthin, ambazo zote ni muhimu kwa afya ya macho pia.

Kabichi ni nzuri pia inapotumika katika kipindi cha baridi ambapo inaweza kutengenezwa kama kachumbali.

Karanga nazo ni miongoni mwa vyakula muhimu katika kipindi cha baridi, hii ni kutokana na uwezo wake wa  kuongeza joto la mwili. Pia karanga ni chanzo kizuri cha vitamin E na B3, halii kadhalika karanga husaidia sana kwa afya ya moyo.

Ulaji wa maboga pia hufaa zaidi katika kipindi cha baridi, huku ikisaidia kuondoa baadhi ya sumu mwilini na kupunguza unene zaidi kwa wale wanene kupita kiasi.

Pia matumizi ya juisi ya maboga ni nzuri zaidi kutokana na kuwa na utajiri wa beta-carotene  pamoja na vitamin E, huku ikisaidia pia kutoa kinga dhidi ya athma.

Viazi vitamu pia ni chakula kizuri sana chenye vitamin nyingi na kizuri sana wakati wa kipindi cha baridi na huongeza joto la ziada mwilini, hali kadhalika viazi ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi yaani ‘fiber’ pamoja na vitamin A, C na madini ya ‘manganese’ na ‘copper’. Unaweza kula viazi hivyo mara baada ya kuchemsha.

Mboga za majani nazo zinapendekezwa kuliwa katika kipindi cha baridi, hususani 'spinachi' ambayo huwa na utajili wa virutubisho vya ‘antioxidants’ na madini chuma . Antioxidants ni chanzo kizuri cha nishati mwilini ambayo husaidia kupunguza hali ya ubaridi mwilini.


Unaweza kuwa karibu nasi kwa kulike page yetu ya facebook iitwayo Mandai Herbalist Clinic- mhc na utakuwa ukifikiwa na taarifa zetu zote kutoka kwetu hususani za kuhusu tiba asilia. Pia unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com 


No comments:

Post a Comment