Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Thursday, 30 April 2015

VYAKULA VINAVYOONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA, CHOCOLATE PIA INAHUSIKA
Kama wewe ni miongoni mwa wale wenye tatizo la kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa basi naamini sehemu hii ni vyema ukaisoma kwani nimekuwekea orodha ya vyakula vitakavyokuongezea mhemko wa kufanya tendo la ndoa.


Ulaji wa karanga ni moja ya njia ya kusaidia kuleta hamu ya kushiriki tendo la ndoa, karanga zinaingia katika orodha hii kutokana na uwezo wake wa kutunza mfumo wa mzunguko wa damu kuwa na afya (vascular system). 

Kwa sababu kuwa na mfumo wenye afya (mzunguko wa damu) katika uke na uume huwezesha mwanaume na mwanamke kupata msisimko wa mapenzi haraka hatimaye tendo la ndoa kuwa zuri, lakini pia karanga zina madini muhimu kama vile magnesium, asidi ya folic na zinc ambayo ni muhimu sana katika uzalishaji wa mbegu za mwanaume.

Vyakula vya nafaka navyo ni muhimu katika hili kutokana na kuwa na nyuzinyuzi (fibre) na sukari ngumu (complex sugar) ambazo husaidia kutunza uzito wa mwili. 

Kwa kawaida nafaka husaidia katika kuzalisha homoni za‘testosterone’ kwenye damu. Lakini pia nafaka huwezesha mtu kuwa na nguvu na hivyo kufika mbali zaidi katika safari ya mapenzi.

Matunda na mboga za majani ni muhimu kwa matokeo makubwa sana katika hamu ya tendo la ndoa kwa njia nyingi.
  
Pia kula matunda na mboga za majani huhakikisha balance ya uzito kwani unene (obesity) kwa wanaume kuna matokeo mabaya katika kuzalisha homeni za testoeterone na hatimaye jogoo kushindwa kuwika.

Soya nayo ni muhimu licha ya kuwa na kiwango kidogo sana cha fat na pia kuwa na kiwango kizuri cha protein, soya zina phytoestrogens ambayo husaidia sana wanawake ambao wamefikia menopause kutengeneza homoni estrogen ya ziada. Husaidia uke kuwa laini (wet, lubricated) mwanamke akisisimliwa wakati wa tendo la ndoa.


Chocolate ina phenyl ethylamine, kemikali ambayo husababisha hisia (feelings) za furaha wakati wa mwanamke au mwanaume kufika kileleni (orgasm)


Karibu Mandai Herbal Clinic, tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment