Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 28 April 2015

WATU WAISHIO VIJIJINI BADO HAWAPATI HUDUMA ZA MSINGI ZA AFYARipoti mpya ya Shirika la Kazi Duniani, ILO inaonyesha kuwa asilimia 56 ya watu wanaoishi vijiini hawana huduma za msingi za afya.Idadi hiyo ni maradufu ya wale wa mijini wasiopata huduma kama hizo. 


Kwa mujibu wa ripoti hiyo iitwayo ushuhuda wa dunia kuhusu ukosefu wa uwiano wa huduma za afya kati ya mijini na vijijini imehusisha mataifa 174, huku  ikiweka bayana kuwa bara la Afrika ndio linaongoza kwani asilimia 83 ya wakazi wake wa vijijini hawana huduma hizo.

Hata hivyo, Shirika hilo la Kazi (ILO) limetupa lawama zake katika uwekezaji mdogo kwenye sekta ya afya kwa miongo kadhaa licha ya kwamba afya ni haki ya msingi ya binadamu na inapaswa kupatiwa wakazi wote bila kujali maeneo wanayoishi. Kama hiyo haitoshi, hata pale kwenye miundombinu ya afya bado wahudumu wa afya nao ni tatizo.

Naye Mratibu wa Sera za Aftya kutoka ILO, Xenia Scheil-Adlung, alisema serikali isitegemee suala la afya kwenye misaada bali iwe haki ya kisheria.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo nchini Somalia, Guinea, Niger na Chad takribani asilimia 99.8 hawapati huduma za afya.

Mandai Herbal Clinic inapenda kukujuza kwamba kama unateseka na magonjwa mbalimbali kwa muda mrefu sasa ni mwisho, unachopaswa kufanya ni kuhakikisha unafika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na upate matibabu sahihi kwa kutumia tiba asilia za mimea na matunda. Wasiliana nasi sasa kwa mawasiliano yafuatayo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 


No comments:

Post a Comment