Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 23 April 2015

WHO: WATOTO DUNIANI HAWAPATI CHANJO YA KUOKOA MAISHA

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeelezea wasiwasi mkubwa lilionao kwamba moja ya tano ya watoto duniani hawapati chanjo ya kuokoa maisha.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa WHO kitengo cha chanjo huko Geneva, Jean-Marie Okwo-Bele, ambapo amesema kuwa vifo milioni 1.5 vya mapema vya watoto vinaripotiwa kila mwaka kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa kutumia chanjo.

Aidha, afisa huyo wa Shirika la Afya Duniani ametoa wito wa kufanyika jitihada za kupunguza ufa uliopo katika chanjo ya watoto baina ya nchi mbalimbali duniani na kuzuia vifo vya watoto vinavyosababishwa na kutopewa chanjo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Duniani, mwaka 2013 karibu watoto milioni 22 hawakupata chanjo inayotolewa baada ya kuzaliwa kama chanjo dhidi ya dondakoo, kifaduro na pepopunda (DTP3).

No comments:

Post a Comment