Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 28 April 2015

YAFAHAMU MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUMLISHA MTOTO
Habari za leo mpendwa msomaji wa www.dkmandai.com, karibu sana katika muendelezo wetu wa kuhakikisha unapata elimu ya afya kila siku ikiwemo tiba asilia.


Leo nimeona tuwakumbuke watoto ili kuwahakikishia usalama wao katika mazingira ya kula.

Ukweli ni kwamba familia nyingi kwa sasa zimekuwa zikiishi na kinadada wa kazi (house girl) ambao ndio kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakishiriki katika kuwatunza watoto nyumbani na kuhakikisha wanakula vizuri na kushinda katika hali ya usalama.

Hivyo ninayofuraha kukumbusha wewe mzazi pamoja na dada wa nyumbani au mlezi mambo haya machache ya kuzingatia katika kuhakikisha usalama wa mtoto wakati wa kula;

Jambo la kwanza hakikisha haumuachi mtoto mdogo na chakula au kinywaji bila uangalizi hata kama ni maziwa ya chupa, kama utasahau na kumuacha mtoto katika hali hiyo huweza kusababisha mtoto akapaliwa.

Pia usimpe mtoto chakula au maziwa akiwa amelala, analia au anacheka huweza kumpalia pia.

Epuka kumpa chakula ambacho kinaweza kumkaba au kumpalia hususani karanga, maindi, zabibu n.k

Kabla ya kumpa mtoto chakula hakikisha umekiangalia joto lake usije ukamuunguza mdomo.

Mbali na hayo yote, pia usafi wa mtayarishaji, mlishaji na mlishwaji ni muhimu sana sana katika afya ya mtoto.

Mandai Herbal Clinic inapenda kukujuza kwamba kama unateseka na magonjwa mbalimbali kwa muda mrefu sasa ni mwisho, unachopaswa kufanya ni kuhakikisha unafika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na upate matibabu sahihi kwa kutumia tiba asilia za mimea na matunda. Wasiliana nasi sasa kwa mawasiliano yafuatayo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment