Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 30 April 2015

ZIFAHAMU DALILI ZA FANGASI SEHEMU ZA SIRI KWA WANAWAKE NA NAMNA YA KUEPUKANA NAZO
Fangasi ya ukeni husababishwa na fangasi aina ya Candida albicans. Ugonjwa huu huitwa vaginal candidiasis kwa kiingereza na ni kati ya magonjwa ambayo husumbua wanawake mara kwa mara.


Fangasi ya ukeni huambukizwa kwa njia ya kutumia vyoo vichafu pamoja na kuchangia nguo za ndani na taulo.

Joto pia unyevu mwingi na nguo za kubana huchangia pia kutokea kwa fangasi ukeni. Ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kwa njia ya ngono.

Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na kutokwa na maji maji meupe mfano wa maziwa kutoka kwenye uke ambayo hayana harufu mbaya, kuwashwa sehemu za siri hasa kwenye uke na mashavu ya uke.

Dalili nyinginezo ni maumivu wakati wa kukojoa kwa baadhi ya wagonjwa. Mara chache hali hii hutokea, ikisababishwa nakuchubuka wakati wa kujiwasha.

Kabla ya kupata matibabu ya tatizo hili ni vyema ukaonana na daktari kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Hata hivyo ili kuepukana na tatizo hili ni vyema kuzingatia usafi wa nguo za ndani kwa kuvaa nguo safi iliyofuliwa kila siku na kuanikwa juani (au kupigwa pasi).

Pia vaa nguo za ndani zilizokauka vizuri. Epuka zenye unyevunyevu au mbichi.
Hali kadhalika ni vizuri ukazingatia usafi wa sehemu za siri na kujikausha vizuri mara baada ya kuoga. Huku pia usafi wa choo ukizingatiwa na kuimarishwa.

Pia unaweza kufika kwetu Mandai Herbal Clinic tukakupatia dawa nzuri ya kumaliza fangasi hao iliyotengenezwa kwa mchanganyiko wa mimea asilia ambayo itaondosha tatizo lako hilo kabisa hata kama lilikuwa ni tatizo sugu kwa muda mrefu, Tunapatikana Ukonga, Mombasa jijini Dar es Salaam. Au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443, Barua pepe dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment