Thursday, 9 April 2015

ZIFAHAMU HIZI MBINU 5 ZA KUONDOA MAKOVU MWILINI, TANGO PIA LIMEHUSIKA
Kuna baadhi ya watu husumbuliwa na shida ya kuwa na makovu sehemu mbalimbali ya mwili.


Kuna hii list ya vitu muhimu unavyoweza kutumia ili kuondoa tatizo hilo la kuwa na makovu.

Tango ni moja ya njia nzuri ambayo husaidia kuondoa makovu, unachopaswa kufanya ni kuponda tango na kisha kutumia mchanganyiko wake kwa kupaka juu ya kovu. Hii husaidia sana kulainisha makovu na ikiwa utatumia kwa muda mrefu huondoa makovu pia.

Aloe Vera pia husaidia kuondoa makovu, kata majani hayo na utumie utomvu wake kupaka katika makovu kisha mara baada ya muda Fulani utaona mabadiliko na itapunguza na kuondoa makovu.

Matumizi ya asali pia husahauriwa katika kuondoa makovu, paka asali juu ya kovu na kuiacha usiku kucha. Rudia mara kwa mara kupaka asali hadi pale kovu litakapotoweka.

Aidha, unaweza kutumia baking soda kidogo na maji sehemu yenye kovu na kuikanda sehemu hiyo kwa dakika moja. Fanya hivyo mara mbili kwa siku. Baada ya muda safisha kwa maji ya vuguvugu halafu paka mafuta ya zaituni.
 
Mbali na hayo, pia jitahidi kupata lishe nzuri bila kusahau matunda na mboga mboga ambavyo ni muhimu kwa ajili ya afya ya ngozi. Hali kadhalika kunywa maji ya kutosha kwani maji pia kulainisha ngozi yako na kufanya makovu kutoka kwa urahisi.

Ikiwa unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo sugu unaweza kuonana na Dk Abdallah Mandai kutoka Mandai Herbal Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Au wasiliana naye kwa namba za simu zifuatazo, 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.  

No comments:

Post a Comment