Thursday, 23 April 2015

ZIFAHAMU NJIA ZA KUKABILINA NA MAUMIVU YA VIUNGO.
Maumivu ya viungo ni moja ya tatizo ambalo huwasumbua watu wengi katika jamii hususani wazee.


Leo Mandai Herbal Clinic inakusogezea hizi njia ambazo husaidia kupunguza tatizo hilo la maumivu ya viungo.

Muarobaini
Andaa majani ya muarobaini kisha yatwange na kukamua ili upate juisi yake robo glasi moja, kisha changanya juisi hiyo na maji ya kunywa glasi 7, utakunywa mchanganyiko huo kwa kutwa nzima hadi yaishe. Fanya hivyo siku 10 hadi 15.

Mdalasini
Chemsha mdalasini na maji glasi nane kisha yaache yapoe , kisha kunywa taratibu kwa kuutwa nzima. Tumia tiba hiyo kwa siku 10 hadi 15 na baadaye utaanza kuona mabadiliko.


Karibu Mandai Herbal Clinic, tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment