Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 9 May 2015

ASALI INAUWEZO WA KUTATUA MATATIZO YETU MENGI SANA YA KIAFYA, LEO INASIMAMA KATIKA KUTATUA TATIZO LA WATOTO KUKOJOA KITANDANI


Tatizo la baadhi ya watoto kukojoa kitandani ni moja ya tatizo, ambalo huwakwaza wazazi wengi na hata watoto wenyewe wenye shida hiyo na mara nyingine huchangia baadhi ya watoto kuanza kuathirika hata kisaikolojia.


Katika hali ya kawaida, mtoto anatarajiwa kuacha kukojoa kitandani anapofikisha miaka miwilii hadi mitatu.

Hata hivyo, kuna sababu mbalimbali ambazo huchangia baadhi ya watoto wengine kuendelea kukojoa kitandani hata baada ya umri huo , moja ya sababu hizo ni pamoja na kucheza sana wakati wa mchana na hivyo kusababisha usiku kulala bila kujitambua.

Huenda weekend hii mzazi umekwazika kutokana na mtoto wako kuamka akiwa amekojoa kitandani, lakini ni vyema ukajaribu njia hizi mbili ili kutatua tatizo la mtoto wako.

Kwanza unaweza kuchukuwa kijiko kimoja cha mezani cha asali, kisha mpe mtoto mwenye tatizo hilo alambe hadi amalize kabla ya kwenda kulala. Endelea tiba hii kwa muda wa mwezi mmoja.

Njia ya pili ni hii ya kuchukuwa vitunguu maji, kisha saga hadi kiwe ujiuji. Baadaye chukuwa kijiko kimoja cha mezani cha kitunguu maji changanya na kijiko kimoja cha chai cha asali, kisha mpe mtoto mara tatu kwa siku kwa muda wa siku 30.

Pamoja na kutumia tiba hiyo, mzazi pia hakikisha mtoto anapata muda wa kupumzika mchana pamoja na kuhakikisha mtoto anywi maji mengi saa chache kabla ya kulala.

Pia jitahidi kujenga utaratibu wa kumuamsha mtoto usiku na kumpeleka kwenda kukojoa, hii nayo itasaidia kuondokana na tatizo hilo kwani ukifanya hivyo kila siku baadaye mtoto atazoea na ataanza kuamka mwenyewe kila siku.

Asante kwa kuendelea kuwa karibu nasi, lakini kama unatatizo lolote la kiafya unaweza kuonana na Mkurugenzi Mkuu wa Mandai Herbal Clinic, Dk, Abdallah Mandai kila siku ya Jumatatu hadi Jumapili ofisi, Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au piga simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment