Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 9 May 2015

BAADA YA EBOLA KUISHA, HIKI NDICHO WALICHOAMUA NCHINI LIBERIA
Liberia ni moja ya nchi ambayo iliathirika sana na ule mlipuko wa ugonjwa wa ebola,

Kwa sasa hali imekaa vizuri na sasa taifa hilo limeanza kampeni ya wiki moja ya kuwapatia watoto zaidi ya laki sita chanjo dhidi ya Polio na Surua.

Kampeni hiyo ambayo inaoongozwa na Wizara ya afya ya nchi hiyo kwa kushirikiano na mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kuhudumia watoto UNICEF na Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na Kituo cha Udhibiti Magonjwa (CDC.)

Awali kampeni hiyo ya aina yake ilitakiwa kufanyika mwaka jana lakini ilisitishwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ambapo Liberia inasema mkwamo huo umesababisha kuwaweka hatarini watoto wengi katika kukumbwa na magonjwa hayo.

Chanjo dhidi ya Polio italenga watoto weneye umri wa chini ya miaka mitano, huku ile ya Surua ni kwa watoto wa kuanzia miezi sita hadi chini ya miaka mitano.

Itakumbukwa kwamba mlipuko wa Ebola uliathiri mifumo yote ya afya ikiwemo utoaji wa chanjo, ikiwemo utoaji wa chanjo hiyo dhidi ya Surua uliporomoka kwa asilimia 45 kati ya Agosti na Disemba 2014 kwa mujibu wa serikali ya Liberia.Shukrani za pekee zije kwako kwa kuamua kutembelea tovuti hii kila wakati, tambua kuwa tunathamini sana uwepo wako msomaji wetu na mdau wetu. Tafadhali endelea kuwa karibu nasi kwa kulike ukurasa wetu wa facebook uitwao Mandai Herbalist Clinic- mhc ili upate taarifa zetu kila wakati

No comments:

Post a Comment