Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 19 May 2015

BAADA YA MVUA KUNYESHA MFULULIZO DSM, LEO KUNA HII TAARIFA KUTOKA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA (TMA)


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua zilizoanza kunyesha mwezi Machi hadi Mei, mwaka huu na kusababisha athari mbalimbali, ikiwamo vifo, upotevu wa makazi na uharibifu wa miundombinu katika Jiji la Dar es Salaam zimefikia ukingoni.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma wa Utabiri wa hali ya Hewa (TMA), Dk. Hamza Kabelwa, ambaye amesema kuwa kwa sasa mvua zitaendelea hadi Mei 20, mwaka huu, lakini katika mikoa ya Pwani Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Pwani, Tanga, na visiwa vya Unguja na Pemba.

Kabelwa alisema kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, mvua zimekwisha na kwamba, zitakazoendelea kwenye maeneo mengine hazitakuwa na kasi kama iliyokuwa Mei 6 na 7, mwaka huu.

Pamoja na hayo Dk. Kabelwa alisema kwa sasa wanafanyia uchambuzi wa mifumo ya hali ya hewa ili kuona hali ya mvua ikoje.

Asante kwa kuendelea kuwa karibu na sisi mdau wetu, tambua tunathamini sana mchango wako na uwepo wako kwetu.

No comments:

Post a Comment