Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 9 May 2015

CHANJO YA MALARIA YAONESHA MAFANIKIO NCHINI KENYA


Majaribio ya chanjo dhidi ya malaria nchini Kenya yameonesha dalili nzuri ya mafanikio.


Wanasayansi watafiti kutoka Chuo kikuu cha Oxford Uingereza wamesajili asilimia 67% ya mafanikio katika majaribio ya chanjo hiyo kwa wakenya 121.

Utafiti huo ni wa pili wa haiba yake katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.

Nalo Shirika la Afya Duniani, WHO limesema kuwa visa milioni 198 vya malaria viliripotiwa mwaka 2013, huku takriban watoto 584,000 wakipoteza maisha yao.

Majaribio ya chanjo nyingine tofauti pia yameonesha mafanikio katika kuwakinga watoto wachanga.

Takwimu zinaonesha kuwa watoto 1,300 wanakufa kila siku chini ya jangwa la Sahara kutokana na ugonjwa huo.

Ajabu ni kuwa hakujakuwa na mafanikio makubwa kuhusu mbinu za kupambana na kirusi kinachosababisha malaria.

Kimsingi watafiti hao wamegundua kuwepo kwa aina nne ya virusi.

Hata hivyo, bado haijabainika iwapo chanjo hiyo itakabiliana na aina zote nne za virusi.

Utafiti huo ambao umekuwa ukiwafuatilia wanaume 121 kwa majuma 8 umegundua kuwa idadi ya virusi vinapungua kwa theluthi mbili.

Pia watafiti hao wamegundua aina ya chanjo inayovamia kirusi ndani ya maini ya mgonjwa.

''Kiwango cha juu cha mafanikio kama tulivyoshuhudia hapa ni ishara nzuri. Tunachohitaji ni utafiti zaidi ili tuwanusuru mamilioni ya watoto wanaoathirika na Malaria,'' alisema Mtafiti mkuu Prof Adrian Hill.

Kimsingi watafiti hao wamegundua kuwepo kwa aina nne ya virusi, huku hatua ya pili ya utafiti huu sasa ikielekea Burkina Faso ambapo utafiti utahusisha watoto.

Profesa Chris Drakeley, kwa upande wake alionya kuwa kunahaja kubwa ya tahadhari maanake huenda madawa haya yakafaa watu wazima ilhali watoto ndio wanaoathirika kwa kiwango kikubwa zaidi.

Hata hivyo Profesa Drakeley, anashauri kinga dhidi ya ugonjwa huu ni kulala ndani ya vyandarua vilivyotibiwa.

No comments:

Post a Comment