Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Tuesday, 12 May 2015

DK MANDAI LEO ANAKUFAHAMISHA KUHUSU MMEA UITWAO HOODIA AMBAO UNAUWEZO MKUBWA KATIKA TIBA IKIWA NI PAMOJA NA KUTIBU SARATANI


Dk, Abdallah Mandai
Habari za wakati huu mpendwa msomaji wetu wa www.dkmandai.com, karibu katika muendelezo wetu wa kufahamishana mambo mbalimbali kuhusu mimea, mitishamba, nafaka na matunda ambayo ni tiba.

Leo hii nakukutanisha na Dk, Abdallah Mandai, kutoka Mandai Herbal Clinic ambao amependa kushare nasi kuhusu mmea huu uitwao Hoodia.

Hoodia ni mmea ambao huenda ukawa si maarufu sana miongoni mwetu, lakini kimsingi ni kwamba mmea huu unawekwa katika kundi la maua na unapatikana sana katika nchi za South Afrika, Botwasana, Namibia, Lesotho pamoja na Swaziland.

Dk, Mandai anasema kwamba, maua ya mmea huu wa hoodia huwa na harufu ambayo si nzuri sana yaani harufu kama ya nyama iliyooza na pale mmea huu unapotoa mbelewele zake basi hupendwa sana na nzi.

Hata hivyo, Dk, Mandai anaeleza kwamba pamoja na hayo, mmea huu umekuwa ni msaada mkubwa kwa baadhi ya watu duniani, huku akitolea mfano nchi ya Namibia ambao wao huutumia mmea huu kama kitulizo cha maumivu mbalimbali ya mwili na kujitibu pale wanapopatwa na maambukizi madogomadogo.
Mmea wa Hoodia


Mmea wa Hoodia
Aidha, anaongeza kuwa baadhi ya watu wazamani maarufu kama (San Bushmen) ambao waliishi katika jangwa la Kalahari wao waliutumia mmea huu katika kuongeza hamu ya kula.

Pia Dk, Mandai anasema matumizi ya mmea huu husaidia sana kwa wale wenye tatizo la unene pamoja na vitambi kutokana na mmea huu kuwa na uwezo mkubwa wa kupunguza unene kwa haraka sana.

Mbali na uwezo huo wa mmea huu, Dk Mandai anasema kikubwa zaidi mmea huo (hoodia) unauwezo mkubwa wa kutibu saratani, na kuondoa mafuta hatari kwenye moyo na huwasaidia sana watu wenye vitambi.

Hata hivyo, anatahadharisha kuwa si kila mtu anaruhusiwa kutumia mmea huu, watu hao ni pamoja na kinamama wajawazito, wale wanaonyonyesha pamoja na watoto. Hivyo anasisitiza kuwa ni vyema kumuona na mtaalam kwanza kabla kuanza kutumia mmea huu kama dawa.

Kama unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo yale sugu tafadhali fanya jitihada za kuonana na Dk, Mandai ili upate suluhisho la tatizo lako la kiafya. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana nasi kwa simu namba, 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment