Friday, 22 May 2015

EBOLA IMETAKIWA KUWA FUNZO KATIKA KUKABILIANA NA MAJANGA

Jamii ya kimataifa imepaswa kubadili haraka na jinsi ya kukabiliana na dharura za kiafya kwa lengo la kuepuka janga jingine kama Ebola.Tahadhari hiyo imetolewa na wataalam wa Shirika la Afya Duniani, WHO ambapo wamesema kuwa mlipuko wa Ebola haujamalizika Afrika ya Magharibi..

WHO imesema mifumo hafifu ya ya afya katika nchi hizo inahitaji uwekezaji mkubwa kutoka nje.

Dr Ruediger Krech kutoka WHO amesema, jamii ya kimataifa ilikimbilia kuuzima moto wa Ebola, lakini imeshindwa kufikiria jinsi ya kuuzuia usiibuke tena.

"Tunasubiri moto uwake, tunakimbia kuuzima, lakini tunasahau kuweka kinga dhidi yake. Tunapaswa kubadili hilo, na tunatoa wito kwa jamii ya kimataifa iunge mkono juhudi za kujikita kwa mfumo wa huduma za afya kwa ujumla badala ya kumulika tu magonjwa makubwa, ili janga jingine kama la Ebola lisitokee tena kamwe."

Katika mkutano na waandishi wa habari, afisa huyo wa WHO amesema ni muhimu kujenga mifumo ya afya Guinea, Liberia na Sierra Leone ambayo ni dhaifu.

Itakumbukwa kwamba mlipuko wa homa ya Ebola umewaua zaidi ya watu 11,100, hususani katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone.

No comments:

Post a Comment