Wednesday, 27 May 2015

FAHAMU JINSI GANI SAMAKI ANAWEZA KUKUFANYA KUONEKANA NA NGOZI NZURI


Matumiani yangu kuwa u mzima mpendwa msomaji wetu wa www.dkmandai.com. Leo pamoja na mambo mengine vyakula vinavyoimaisha afya ya ngozi, karibuni

Vyakula vya baharini ni miongoni mwa vyakula muhimu sana katika kuimarisha afya ya ngozi.

Vyakula hivi hufaa kwa afya ya ngozi kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha Zinc na Omega 3 ambazo ni muhimu kwa siha ya ngozi.

Faida za Omega 3 ni pamoja na kuondoa kukakamaa au ukavu wa ngozi na kupunguza kuvimba na kukunjamana kwa ngozi.

Pia husaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini hivyo kuboresha ngozi. Damu inapozunguka vyema mwilini afya ya ngozi nayo huimarika. Zinc nayo husaidia kuondoa harara na chunusi katika ngozi kwasababu huyeyusha homoni ya testosterone. Pia husaidia kuzalishwa seli au chembe hai za mwili na kuondoa chembe zilizokufa huku ikiifanya ngozi ing'ae na kuwa na mvuto zaidi

Kama unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo yale sugu, hebu fanya utaratibu wa kufika ofisini kwetu ili tuweze kutatua tatizo lako la kiafya vizuri kabisa. Pia unaweza kututafuta kwa mawasiliano yafuatayo 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300 Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Pia namba hizo za simu zimeunganishwa na whatsapp. Kwa wale wa facebook tupate kupitia ukurasa wetu uitwao Mandai Herbalist Clinic- mhc.

No comments:

Post a Comment