Thursday, 21 May 2015

FAHAMU KUHUSU TATIZO LA KUPOTEA KWA NYWELE (KIPARA)


Tatizo la upotevu wa nywele ni tatizo ambalo huwakumba baadhi ya watu na kuwakosesha raha kabisa, hivyo leo nimeona ni vyema tuzungumzia tatizo la upotevu wa nywele.


Na kama ulikuwa hujui basi fahamu kuwa nywele za kichwani zina uimara wa ajabu na ukweli ni kwamba unywele mmoja unaweza kuvuta uzito wa gram 100.

Kwa wastani nywele hukua kwa sentimita 1 kila mwezi na kiwango kikubwa cha ukuaji huwa kati ya miaka 15 na 30. Unywele mmoja unauwezo wa kudumu kwa miaka 4.


Wataalam wanakiri kwamba wastani wa ncha 100 za nywele hupukutika kwa siku na nywele mpya hujitengeneza katika kipindi cha wiki 6 hadi 10.

Hatutakuwa na makosa kama tukisema nywele zetu hujitengeneza upya kila wakati. Tatizo linakuja pale ambapo nafasi ya nywele zinazoondoka haizibwi na mpya.

Kipara ni moja ya matatatizo ambayo yanawakumba wanaume tangu hapo kale kutokana na ukosefu wa nywele.

Kunaweza kuwa na sababu nyingi zinazosababisha upotevu wa nywele kwa wanawake na wanaume.

Baadhi ya sababu ni pamoja na utumiaji wa madawa, kumalizika kwa kipindi cha uzazi kwa wanawake (yaani menopause), upungufu wa madini ya chuma na zinki, upungufu wa protini, kunywa pombe na uvutaji tumbaku.

Lakini endapo kama upotevu wa nywele unasababishwa na chanzo kimoja tu, tatizo hili huweza kutibiwa kama hicho chanzo kitadhibitiwa.

Mfano mkubwa wa upotevu wa nywele ni upara kwa wanaume. Upotevu huu wa nywele ni jinamizi kubwa sana kwa wanaume. Japo kuna mambo mengine yanayosababisha tatizo hili, lakini chanzo kikuu ni la kijenetiki.

Tatizo la upara kwa wanaume ambalo pia husababishwa na homoni, huanzia mbele ya kichwa kuelekea kisogoni. Kila kinavyoendelea kuongezeka, ukingo mdogo wa nywele hubaki pembeni na nyuma ya kichwa.

Ingawa kasi ya upotevu wa nywele huweza kupunguzwa kwa kutumia dawa za kumeza na vipodozi vinavyopakwa kichwani, lakini haiwezekani kusitisha kabisa tatizo hili.

Baadhi ya wanaume hukubaliana na tatizo hili, na wengine hawakubaliani nalo na huwasumbua sana mpaka kupata matatizo ya kisakolojia.

Njia ya upandikizaji wa nywele imekua ni njia ambayo wengi waliosumbuliwa sana na tatizo la upara wanaitumia. Upandikizaji wa nywele ulifanywa kwa mara ya kwanza mwaka 1939 na daktari bingwa wa dermatology, dokta S. Okuda mwenye asili ya Kijapan.

Njia hii ilikuja kuwa maarufu mnamo mwaka 1970 wakati daktari wa dermatolojia kutoka Marekani, Norman Orentreich alipogundua njia nyingine.

Mambo mengi sana yanabidi yazingatiwe yakiwemo rangi ya mywele na aina ya nywele, rangi ya ngozi na aina ya ngozi ya mhusika.

Nchi ya Uturuki inaongoza katika ukanda kwa utumiaji wa njia endelevu za upandikizaji nywele.

Vituo vingi vya afya vinafanya upandikizaji wa nywele katika bei nafuu kwa kutumia wataalam wenye uzoefu wa kutosha kwa wagonjwa wengi kutoka ndani na nje ya nchi.

Bei zake ni kati ya Euro 1000 na 2500 kulingana na aina ya upandikizaji ambao mgonjwa atafanyiwa.


Ikiwa ungependa kufika Mandai Herbalist Clinic na kufahamu mengi zaidi kuhusu mimea tiba, mitishamba, nafaka  na matunda ni vyema ufanye mawasiliano nasi kupitia 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Namba zetu hizo pia zinapatikana kwenye whatsapp. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam  

No comments:

Post a Comment