Friday, 22 May 2015

FAIDA ZA KUTUMIA MAFUTA YA NAZI


Nazi ni moja ya kiungo kizuri ambacho mara zote tumekuwa tukitumi katika vyakula.

Leo napenda kushare na wewe msomaji wetu wa www.dkmandai.com kuhusu faida za mafuta ya kiungo hiki (nazi).

Mafuta ya nazi yana faida nyingi katika mwili wa mwanadamu, kwanza kabisa mafuta ya nazi yana uwezo mkubwa sana wa kuharibu aina zote za bacteria na virusi hatari kwa ustawi wa afya ya mwanadamu.

Karibia asilimia hamsini ya mafuta ya nazi ni lauric acid ambapo mwili wa mwanadamu hubadili lauric acid kuwa monolaurin. Hii monolaurin ni aina ya monoglyceride ambayo ina uwezo mkubwa sana wa kupambana na nguvu ya virusi.

Pia mafuta ya nazi husaidia kuimarisha mfumo wa mmen’genyo wa chakula katika mwili wa mwanadamu.

Pamoja na hayo, mafuta ya nazi huimarisha afya ya moyo wa mwanadamu, huku yakisaidia pia kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili

Mbali na hayo, matumizi ya mara kwa mara ya mafuta ya nazi husaidia katika kuifanya ngozi ya kuwa yenye afya njema na kumfanya muhusika kuonekana kijana.

Unaweza kuwasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic kwa mawasiliano yafuatayo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment