Friday, 29 May 2015

FAIDA ZA MATUMIZI YA MCHICHA


Mchicha ni mboga maarufu sana miongoni mwa watanzania wengi na ni moja ya mboga ambayo hataupatikanaji wake ni rahisi pia.

Mbali na mboga hii kuwa ni maarufu, lakini pia mchicha ni tiba ya matatizo mbalimbali ya kiafya.

Moja ya matatizo hayo ni pamoja na matatizo ya maumivu ya mgongo.

Ili kutibu tatizo hilo mhusika anapaswa kutafuta mchicha na kuupondaponda kisha kuutumia kwa kujichua sehemu ya mgongo yenye maumivu. Fanya hivyo mara tatu kwa siku.

Lakini pia wakati wa usiku kabla ya kulala unaweza kupasha moto mchicha na kufunga mahali pale panapouma. Kisha lala nao wakati ukiwa na uvuguvugu wake. Fanya hivyo kwa siku 5.

Pia ulaji wa mchicha mara kwa mara huweza sana kumsaidia mtu kuongeza damu mwilini

Unaweza kuwasiliana nasi kwa mawasiliana yafuatayo: 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300 Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri na matibabu ya magonjwa mbalimbali sugu.

No comments:

Post a Comment