Saturday, 16 May 2015

FAIDA ZA MBEGU ZA TIKITI MAJI ZIMEULIZIWA SANA, KUTOKANA NA UPENDO WETU KWAKO MDAU WETU TUMEAMUA KUKUWEKEA HAPAHabari za wakati huu mdau wetu wa www.dkmandai.com karibu sana tufahamishane mengine kuhusu masuala ya afya na tiba asilia kwa ujumla.


Jumamosi hii nimepokea maombi kutoka kwa mmoja wa wadau wetu wa karibu sana aitwaye Clifford Hezron ambaye amekuwa akitufuatilia kwa karibu kila siku, yeye alinitumia ujumbe kupitia ukurasa wetu wa facebook uitwao Mandai Herbalist Clinic- mhc ambapo aliomba kufahamu faida za mbegu za tikiti maji pale zinapoliwa.

Hivyo nimeona ni vyema kwa faida ya wengine pia, ambao nao wangependa kufahamu faida za tunda hili ni vyema tuzungumzie kupitia tovuti yetu hii ya www.dkmandai.com

Tikiti maji ni moja ya tunda lenye kiwango kikubwa cha maji, lakini pia ukipata ambalo zuri yaani lile ambalo limekomaa vizuri huwa na ladha nzuri zaidi.

Lengo letu leo ni kuzungumzia faida za mbegu zake, ambapo miongoni mwa faida za kutumia mbegu hizo ni pamoja na kusaidia sana kushusha shinikizo la damu.

Pia mbegu za tunda hili huweza kutumika kama msaada kwa wale wenye shida ya kupata maumivu wakati wa kutoa haja ndogo (kukojoa) .

Mtu mwenye shida hiyo anatakiwa kuchukua kiasi cha mbegu za tikiti maji na kuzikaanga kisha kuzisaga na kutumia unga huo.

Tumia unga huo kwa kuchanganya na maji kisha tumia vijko viwili kutwa mara mbili.

Mbali na hayo kimsingi ulaji wa mara kwa mara wa tunda hili huweza kusaidia sana kukulinda dhidi ya magonjwa kama baridi yabisi, matatizo y figo, kupunguza unene, maumivu ya viungo, tumbo pamoja na shida ya usagaji wa chakula.

Pia katika tikiti maji kuna vitamin A, ambayo husaidia kuboresha afya ya macho na kuondosha sumu mwilini.

Nawe pia unaweza kutuambia chochote kupitia ukurasa wetu wa facebook uitwao Mandai Herbalist Clinic- mhc. Au barua pepe: dkmandaitz@gmail.com. Tupigie simu namba zifuatazo, 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe,


No comments:

Post a Comment