Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 7 May 2015

HALI YA JIJI LA DSM MAENEO YA BUGURUNI HAIKUWA SHWARI KUFIKIA MCHANA WA LEO, NYUMBA ZIMEZINGIRWA NA MAJI KILA KONA, KUNA PICHA HAPA

Baada ya mvua kunyesha usiku mzima wa jana nakuendelea siku ya leo, kamera yetu ya www.dkmandai.com ilifika maeneo yake Buguruni, faru ambapo tulishuhudia nyumba nyingi za wakazi wa eneo hilo zikiwa zimezingirwa na maji.


Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa hali ni mbaya sana ndani ya makazi yao na tayari vitu vyao vya umeme vimeharibika pamoja na magodoro na hawaelewi nini cha kufanya, kwani tangu usiku wamekuwa wakihangaika kutoa maji,lakini bado yamekuwa yakizidi kuongezeka kila wakati.

Picha zifuatazo ni madhara ya mvua inayoendelea kunyesha hii ni maeneo ya Buguruni
Mpigapicha nami ilinilazimu kupandisha suluali yangu ili kupata baadhi ya picha, hapa nilikuwa nikipita ndani ya maji huku nikipiga picha hawa wakazi wakivuka eneo lililoja maji lililopo nyuma ya viwanda vilivyopo eneo la mchicha karibu na Tazara jijini Dar es Salaam


Mtoto huyu tulimkuta akiogelea bila kujali usalama wa maji haya
Kutokana na kuthamini afya na kutambua kuwa maji hayo ni machafu na yanaweza kumletea madhara kiafya ilibidi kumkemea kidogo na hapa akawa anakimbia baada ya kumkemewa.

Mabinti hawa walikuwa wakivuka maji hayo kwa kupima kina cha urefu kwa kutumia fimbo kwanza ili kuepuka ajali
Hata hivyo,  Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini imearifu kuwa mvua hizo bado zitaendelea leo na kesho, hivyo tahadhari zaidi imetakiwa kuendelea kuwepo miongoni mwa watanzania wa maeneo mbalimbali  hapa nchini

Mandai Herbalist Clinic tunatoa pole zetu za dhati kwa wale wote ambao wameathiriwa na mvua hizi zinazoendelea kunyesha hapa nchini katika maeneo mbalimbali ikiwemo jijini Dar es Salaam na Zanzibar.

No comments:

Post a Comment