Thursday, 21 May 2015

HAYA NDIYO MADHARA YA PARACETAMOL KATIKA UWEZO WA KUZALISHA


Wanawake wajawazito wametakiwa kuchukua tahadhari zaidi wanapotumia dawa zozote zilizo na chembechembe za Paracetamol.


Kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi nchini Uingereza umebaini kuwa unywaji wa dawa zenye kiungo cha Paracetamol kwa kipindi cha siku saba hupunguza uwezo wa uzalishaji wa homoni za kiume ''testosterone''.

Homoni hiyo ''testosterone'' ndio inayowezesha kuumbwa kwa sehemu ya uzazi wa kiume .

Madaktari wameshauriwa kutowapatia dawa zenye ''Paracetamol'' kwa wanawake waja wazito kiholela.

Na iwapo itawalazimu kuwapatia dawa hizo dawa hizo basi wanashauriwa kuwapa dawa hizo kwa kipindi kifupi ilikupunguza madhara kwa watoto waliotumboni.

Pamoja na hayo nayo halmashauri inayosimamia matumizi ya madawa nchini Uingereza sasa imesema licha ya kuwa inahujumu kiumbe kilichoko tumboni, Paracetamol ni moja kati ya madawa yenye madhara machache zaidi kwa mama mjamzito na mwanawe.

Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa onyo kutolewa dhidi ya wanawake wajawazito kupewa dawa zilizo na kiuongo cha Paracetamol.

Hapo awali utafiti wa wanawake wajawazito 2,000, nchini Denmark ulibaini kuwa,wanawake waliomeza dawa za Paracetamol walijifungua watoto waliolemaa katika sehemu ya mfuko wa uzazi korodani.

Ulemavu huo hatimaye ulijitokeza na kuwa upungufu wa uwezo wao kuzalisha katika maisha yao ya utu uzima.

Aidha inasemekana kuwa wanawake wanaotumia dawa hiyo yakupunguza maumivu kwa kipindi kirefu wakati wa ujauzito, wanaweza kuathiri mimba zao na hasa kwa watoto wakiume.

Wanasayansi hao wa Chuo kikuu cha Edinburgh, walitumia panya katika utafiti huo.

Utafiti huo ulifaulu baada ya madaktari kuwapasua panya na kuwapandikiza mimba na kisha wakawapa dawa hiyo kwa siku saba.

Shirika linalosimamia maswala ya afya Nchini Uingereza, linasema kuwa wanawake wajawazito wanafaa kumeza tembe hiyo ya paracetamol ikiwa tu wameshauriwa na daktari na pia kwa kipindi kifupi mno.

Dr Rod Mitchell, aliyeongza utafiti huo anasema kuwa tahadhari kubwa inapaswa kuwekwa inapowadia swala la matumizi ya Paracetamol miongoni mwa wanawake wajawazito.

Hata hivyo, watafiti hao wanasema ni vigumu kubaini iwapo athari hiyo ni sawa sawa miongoni mwa wanadamu.

Licha ya utafiti huu msemaji wa chuo cha afya ya watoto nchini Uingereza Dr Martin Ward-Platt, anaonya kuwa wanadamu hawapaswi kukatazwa kabisa kumeza dawa zilizo na Paracetamol kwa sababu zinasaidia sana kutibu mafua ya mara kwa mara na wakati mwengi kipimo kimoja au viwili vya Paracetamol vinatosha kutibu homa.

Daktari Sadaf Ghaem-Maghami, kwa upande wake ameonya kuwa utafiti huo haupaswi kukubalika pasi na maswali muhimu kuulizwa kuhusu ukweli wake.

''Licha ya kuwa matokeo ya utafiti huu ni mzuri na unavutia ,tunapaswa kufanya utafiti zaidi kwa sababu utafiti huu ulifanyiwa wanyama, Je mwili wa binadamu utaitikia vipimo vya dawa hii kwa njia sawa na hiyo ? alihoji dakta Sadaf.

Utafiti huo umechapishwa katika jarida la kisayansi na utabibu '' Translational Medicine''.

Sisi Mandai Herbal Clinic tunapenda kukwambia kuwa unaweza kuepuka madhara kama hayo kwa kujenga utamaduni wa kupenda kutumia tiba asilia ambazo hazina chembe hata moja ya kemikali.

No comments:

Post a Comment