Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 12 May 2015

HII NI MAHUSUSI KWA WEWE MWANAMKE AMBAYE UNAPENDA UREMBO, ANZA KUISHI HIVI SASA
Masuala ya urembo ni moja ya mambo yenye dhana pana kidogo kwani urembo unajumuisha mambo mengi kwa mwanamke tofauti na watu wengi wanavyodhani.

Baadhi hudhani urembo ni kuonekana vizuri, kuvaa vizuri, kujipulizia manukato mazuri, kuwa na umbo zuri, na jinsi unavyoonekana kutokana na umbo lako. Kimsingi hivyo vyote ni vidokezo au dondoo za urembo kwa mwanamke.
 
Urembo halisi ni amani na utulivu uliopo ndani ya mtu husika, hali hii huwa na faida katika moyo wako na mwili wako pia.

Jambo la msingi hapa ni kuwa na amani kwa kuepuka msongo wa mawazo na kuwa mwenye furaha muda wote.

Kuwa na msongo wa mawazo (stress) huleta maradhi mbalimbali kama vidonda vya tumbo (gastric ulcers), shinikizo la damu (blood pressure) na mengine mengi.

Katika maisha ya mwanamke yeyote mwenye kupenda urembo na muonekano mzuri ni pamoja na kuepukana na magonjwa yanayoepukika kwa njia rahisi ya kuwa na amani na furaha muda wote kwa kujenga sura nzuri, umbo zuri lenye kupendeza pale unapovaa nguo ya aina yoyote au kupaka vipodozi vya aina yoyote ile.
 
Jiulize ni kiasi gani cha fedha huwa unatumia kila mwaka kununua vipodozi, viatu, nguo mpya pamoja na mikoba. Bila shaka ni gharama kubwa lakini je, kuna gharama gani itatumika endapo ukiamua kujenga furaha na amani ndani yako? Jibu ni rahisi tu furaha na amani ni wewe mwenyewe pasipo gharama yoyote ile.

Zifuatazo ni dondoo muhimu zitakazo ongeza urembo wako wewe mwanamke.

Kupata muda wa kutosha wa kupumzika Inafahamika kwamba wanawake hutumia muda mwingi kutimiza majukumu ya kifamilia kama mama, dada, watoto wa kike, lakini yatupasa kupata muda wa kupumzika na kupata hewa safi kila baada ya shughuli mbalimbali za kila siku ili kujenga afya ya ngozi yako kimuonekano na akili pia.

Mazoezi ni muhimu katika urembo, 
Kufanya mazoezi kutakupunguzia uchovu na uzembe wa mwili, na hivyo kuuandaa mwili kupambana na magonjwa mbalimbali kama mafua na maumivu ya mwili.

Mazoezi pia yanajenga umbo zuri kwa mwanamke kwa kupunguza mafuta mwilini na hivyo kuleta muonekano mzuri hata unapovaa nguo yako na kuvutia.

Kunywa maji ni muhimu.  
Katika kuongeza urembo wa ngozi yako maji ni muhimu pia kwani yanasaidia kuboresha tishu za ngozi na kufanya ngozi isiwe kavu kwa kuongeza unyevu katika ngozi.

Pia endapo ngozi yako ni ya mafuta zaidi unashauriwa kujizoesha kunywa maji yenye vuguvugu ili kupunguza mafuta.

Ishi ukiwa na tabasamu kila mara.  
Katika hili jifunze kusaidia wengine wenye matatizo kwa kuwapa tabasamu, hii itajenga urafiki na watu tofauti na hivyo kupelekea amani na furaha kati yenu. Itakupa ujasiri kama mwanamke na kuwa kioo cha jamii kwa kusaidia wenye matatizo.

Kaa mbali na majungu Mara nyingi majungu hupelekea ugomvi na hasira na hivyo kupelekea sura kukunjamana na kukosa amani pia. Hivyo kwa kuepuka hali ya ugomvi itajenga furaha wakati wote na sura yenye tabasamu hivyo urembo wa nje utajitokeza kirahisi zaidi.

Zingatia kwamba suala la kuwa mrembo lipo mikononi mwako kwani furaha ya mtu huletwa na mtu mwenyewe basi jenga tabia ya kujipa furaha mara kwa mara na kujiaminisha kiakili na utakuwa mwenye ngozi nzuri kama mwanamke na afya njema. 

Tunapenda kuendelea kukukaribisha Mandai Herbal Clinic, endapo unasumbuliwa na matatizo mbalimbali ya kiafya, tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Au wasiliana nasi kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment