Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 5 May 2015

HIVI UNAFAHAMU KAROTI INAPOCHANGANYWA NA GILIGILIANI INAWEZA KUWA TIBA NZURI YA TETEKUWANGA?
Tetekuwanga au ‘chickenpox’  kwa lugha ya kiingereza huu ni ugonjwa ambao hautofautiani sana na surua kutokana na ugonjwa huu nao kuwashambulia sana watoto wenye umri wa chini ya miaka saba.


Ugonjwa huu unaambukiza kwa haraka sana, hususani pale ambapo unaonekana kwamba unaelekea kupona.

Dalili za tetekuwanga ni pamoja na hali ya kuhisi  kuwa na homa, kuumwa kichwa, kusikia uchovu wa mwili, kuonekana kwa vipele kifuani aua sehemu ya juu ya mgongo na hatimaye upele unaofanana na malengelenge husambaa mwili mzima.
 
Muonekanano wa mgonjwa mwenye tetekuwanga
Hata hivyo, baada ya siku chache upele huo hutumbuka na kuanza kukauka na hapo mgonjwa  huweza kuanza kupona kwa kipindi cha siku kumi hadi ishirini.

Ugonjwa huu wa tetekuwanga ni ugonjwa unaoenea kwa njia ya virusi

Moja ya tiba asilia inayoweza kutoa ahueni kwa mtu mwenye tetekuwanga  ni kutumia giligiliani ambapo inapaswa kupondwa pamoja na karoti na kuchanganywa na maji kisha chemsha kwa dakika 10 na uchuje na kunywa maji yote kwa siku moja. Endeleza tiba hiyo kwa siku nne.

Kwa maelezo zaidi karibu Mandai Herbal Clinic, tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment