Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 8 May 2015

HUU NDIO UAMUZI ULIOAMULIWA NA SERIKALI YA IVORY COAST KUHUSU MATUMIZI YA MIKOROGO


Ivory Coast imepiga marufuku uingizwaji, uuzaji na usambazaji wa bidhaa zozote zenye uwezo wa kuchubua rangi ya ngozi ya binadamu .

Katika taarifa kwa vyombo vya habari Wizara ya afya ya nchi hiyo imetangaza kuwa ni haramu kuingiza bidhaa hizo katika namna yeyote iwe ni vipodozi ama matembe kwa sababu ya athari zake kwa afya.

Taarifa zinasema kuwa bidhaa nyingi za kijichubua rangi ya ngozi zinauzwa katika taifa hilo la Magharibi mwa Afrika.

Marufuku hiyo inaharamisha uingizwaji wa vipodozi , mafuta, na tembe zenye madini ya zebaki na vyuma vinavyotumiwa kuchubua rangi pamoja na kemikali zingine.

Kulingana na afisa wa halmashauri inayosimamia matumizi ya madawa nchini humo Christian Doudouko amesema kuwa, idadi ya watu ambao sasa wanaonesha dalili za kuathirika kiafya na madawa hayo ya kuchubua ngozi imeongezeka mno katika miaka ya hivi punde na kulazimisha wizara ya afya kuchukua hatua hiyo kali.

Afisa huyo aidha alisema kuwa madini hayo haswa ya zebaki yanaweza kusababisha maradhi ya saratani ya ngozi.

Naye daktari Elidje Ekra, alisema kuwa kemikali zinazotumika ilikuhakikisha ufanisi wa kuchubua rangi asili ya binadamu zinachangia kwa kiasi kikubwa kuzuka kwa matatizo ya shinikizo la damu pamoja na hata kisukari.

Daktari Ekra ambaye pia ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Treichville Abidjan anasema ameshuhudia magonjwa mengi tu ya ngozi yasiyo na tiba na kila alipofanya upelelezi aligundua kuwa wagonjwa walikuwa pia ni watumizi wa mikorogo.

Mikorogo hiyo ya kujichubua ngozi na maarufu mno katika mataifa mengi ya Afrika huku wanawake wengi wakipendelea kujichubua iliwakubaliwe kuwa ni warembo.

Hayo yote yanakuja kufuatia kasumba ya dhana ya wanawake kuamini kuwa urembo ni sharti uwe na ngozi laini na nyeupe.

Matumizi ya mikorogo sasa hata imeanza kupata umaarufu miongoni mwa baadhi ya wanaume.

Licha ya kutokuwepo na takwimu maalum kuhusu matumizi ya mikorogo hiyo, mabango ya mauzo na kunadi bidhaa zenye uwezo wa kukufanya uwe ''Mrembo'' zimezagaa kote barani Afrika.

Hata hivyo, kufuatia tamko hilo la serikali huko nchini Ivory Coast bado haijajulikana hadi sasa wanawake wanotumia mikorogo wamechukulia vipi kauli hiyo ya serikali.

No comments:

Post a Comment