Monday, 25 May 2015

IFAHAMU TIBA YA MGUU ULIOTEGUKA AU KSHITUKA


Habari za Jumatatu mpendwa msomaji wetu wa www.dkmandai.com karibu katika muendelezo wetu wakufahamishana mambo mbalimbali kuhusu tiba asilia na mimea mbalimbali kwa ujumla.

Leo nimeona ni vyema tujuzane kuhusu hii mbinu ya asili inayoweza kukusaidia pale unapopata uvimbe kutokana na kuumia, kuteguka au kushituka.

Inawezekana umewahi kuumia au mtoto wako amewahi kuteguka kutokana na michezo na ukajikuta akipata uvimbe , lakini ukashindwa ni mbinu gani utumie ili kupunguza uvimbe ukiwa bado nyumbani kwako.

Sasa leo kuna hii njia unayoweza kuitumia na ikakusaidia sana kuondosha uvimbe wa sehemu iliyotokana na kuumia kwa kuteguka au kushituka unachopaswa kuwa nacho ni ukwaju pamoja na chumvi tu, ili kukamirisha tiba hii.

Kamua ukwaju ili kupata juisi yake nzito, kisha ongeza chumvi nyingi na ukoroge vizuri kisha mchanganyiko wako huo ukishachanganyika vizuri utautumia kwa kupaka sehemu zote zenye uvimbe uliotokana na kuumia au kuteguka.

Baada ya kupaka, utaacha mchanganyiko huo hapo hapo. Baada ya saa 12 paka tena, endelea hivyo hivyo hadi pale utakapoona uvimbe utakapokuwa umepungua kiasi cha kutosha au kuwa katika hali ya kawaida.

Kwa ushauri na matibabu zaidi ya magonjwa mbalimbali, tafadhali fika ofisini kwetu Mandai Herbalist Clinic iliyopo, Ukonga jijini Dar es Salaam. Au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo: 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment