Saturday, 2 May 2015

JE, INAPOTOKEA UKATUFUNA MBEGU ZA MACHUNGWA KUNAMADHARA?
Chungwa ni tunda linalosifika kuwa na vitamin nyingi hususani vitamin c, lakini wengi wamekuwa wakijiuliza je nini kinaweza kutokea endapo mtu atatafuna mbegu za machungwa.


Mbegu za machungwa hasa zile zilizochungu kama zilivyo mbegu za matunda ya epo, zina kiasi kidogo cha sumu aina ya cyanide.

Aina hii ya sumu ikiliwa kwa wingi inadhuru afya. Ndio kusema, kutafuna mbegu nyingi za machungwa ni ulaji usiofaa wa matunda hayo.

 Tabia hiyo inaweza kumsababishia mtu matatizo ya kiafya kwa maana mrundikano mkubwa wa sumu hiyo huathiri mwili.

Mbegu za machungwa kutokana na wingi wake wa virutubisho kama protini, vitamini, madini, mafuta na nyuzinyuzi, zinatumika katika viwanda kutengeneza bidhaa mbalimbali zikiwamo mafuta, dawa, chakula cha ngo’mbe na mbolea.

Chanzo: Mwananchi.

No comments:

Post a Comment