Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 13 May 2015

JE, NI MARA NGAPI UMESHAJARIBU KUTUMIA KARAFUU ILI KUMALIZA MATATIZO YAKO YA MENO?


Habari za leo mpendwa msomaji wetu wa www.dkmandai.com, matumaini yetu ni mzima wa afya na umeanza shughuli zako vyema, licha ya kuendelea kuwepo kwa mvua kwa wewe mkazi wa jijini la Dar es Salaam.

Siku ya leo napenda kuongea machache kuhusu faida za kutumia karafu., hiki ni kiungo ambacho hutokana na mmea wa mkarafuu.

Matumizi ya karafuu huweza kuleta matokeo mazuri zaidi kwa wale wenye matatizo ya meno kwani husaidia kuimarisha meno na kuua vijidudu vinavyopatikana kwenye meno pamoja na kuondoa harufu mbaya kinywani.

Pia karafuu husaidia sana kuzuia damu kutoka kwenye fizi, unaweza kutumia karafuu kwa kupenda kutafuna angalau asubuhi na jioni ili kupata matokeo mazuri zaidi kwa kinywa chako.

Acha kuteseka na magonjwa anza kupenda afya yako kwa kufika Mandai Herbal Clinic sasa tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam . Tupigie simu namba zifuatazo, 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment