Tuesday, 26 May 2015

JE, UMEIPATA HII TAARIFA YA WATU 430 KUPOTEZA MAISHA KUTOKANA JOTO


Kuna majanga mengine ni hatari sana na pale yanapotokea huweza kusababisha vifo vya watu wengi zaidi.

Mara kadhaa tumekuwa tukisikia majanga mbalimbali yakiwemo majanga ya njaa, matetemeko ya ardhi, mafuriko, kimbunga pamoja na tsunami.

Sasa huko nchini India watu 430 wamekufa kutokana na nchi hiyo kukubwa na joto kali

Kufuatia tukio hilo maafisa wa utawala nchini humo wamelazimika kuanzisha kampeni ya kuwahamasisha wananchi kukaa majumbani mwao na kuwashauri wanywe waji mengi.

Kufuatia hali hiyo vifo vingi zaidi vimeripotiwa katika majimbo ya kusini ya Telangana na Andhra Pradesh, ambapo watu 140 wamepoteza maisha yao kuanzia Jumamosi wimbi hilo la joto lilipotokea.

Watafiti wamesema kiwango cha juu mno cha nyuzijoto 48'C katika maeneo mengi nchini humo

Wenyeji wameshauriwa kunywa maji mengi mara kwa mara

"Asilimia kubwa ya wale waliopoteza maisha ni watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50 walioshinda nje ya majumba yao.'' alisema Kamishina wa Kupambana na Majanga katika Jimbo la Andhra Pradesh.

Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa nchini humo imesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa hali hiyo ya joto kuendelea kwa siku kadha zijazo, huku idara hiyo ikisema kuwa hali hiyo ya juu ya joto inatokana na ukosefu wa mvua. Hivyo wenyeji wameshauriwa kuendelea kukaa ndani na kunywa maji meng.


Pamoja na hayo, nao madereva teksi ambazo hazina kiyoyozi hawataruhusiwa kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria. Hii inafuatia vifo vya madereva wawili.

Chanzo: BBC Swahili

No comments:

Post a Comment