Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 13 May 2015

JE, UMEKUWA UKISUMBULIWA NA TATIZO LA MIGUU KUPATA GANZI? KUNA HII NJIA HAPA HUENDA ITAKUWA MSAADA KWAKO


Ni Jumatano nyingine tena ya Mei,13, 2015 ambapo tuanakutana kuendeleza utaratibu wetu wa kufahamishana mambo mbalimbali hususani kuhusu afya zetu.

Matumaini yangu mzima wa afya na unaendelea vyema na shughuli zako za kila siku za kujipatia mkate wa siku.

Leo nimependa kuzungumzia namna ya kujitibu tatizo la miguu kuwa na ganzi, moja ya tatizo ambalo huwasumbua watu wengi katika familia zetu au jamii tunazoishi na hasa wale wenye umri mkubwa na wenye uzito zaidi.

Kutokana na kutambua kuwa, hili ni tatizo ambalo huwakabili mama zetu wengi na baba zetu wengi ninapenda kukufahamisha kwamba kitunguu swaumu huenda kikawa suluhisho lako la tatizo hilo.

Unachopaswa kufanya ni kupata punje 5 za kitunguu swaumu na uchanganye na maji lita moja kisha chemsha maji hayo yakiwa pamoja na kitunguu swaumu.
Kitunguu swaumu
Baada ya kuchemka vizuri yaache yapoe, kisha mhusika yaani yule mtu mwenye shida ya kupata ganzi miguuni atumie mchanganyiko huo ndani ya wiki 3 hadi 4 mfululizo.

Jambo la msingi hapa ni kuhakikisha kuwa kila lita moja ya mchanganyiko huo inatumika na kuisha ndani ya siku moja na si vinginevyo, lakini kama ungependa kupata dawa ya tatizo hilo ambayo tayari tumeshaiandaa kutoka hapa ofisini kwetu Mandai Herbal Clinic unakaribishwa sana tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam . Tupigie simu namba zifuatazo, 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment