Monday, 25 May 2015

JE, UMEWAHI KUFIKIRIA MAGANDA YA VIAZI MVIRINGO KUWA TIBA?


Hivi ni mara ngapi nyumbani kwako umepika viazi mviringo na kuyatupa maganda ya viazi hivyo mara baada ya kumenya pasipo kujua kuwa maganda hayo yanaweza kuwa moja ya tiba ya tatizo lolote katika mwili wa binadamu.

Najua unaweza ukashangazwa nah ii tiba ya maganda ya viazi mviringo na utakuwa ukijiuliza ni kwa namna ganiyanaweza kuwa tiba na kama haitoshiutakuwa ukijiuliza je, yanaweza kuwa tiba ya ugonjwa gani.

Lakini usipate tiba Mandai Herbalist Clinic ipo kwa ajili yako na leo inapenda kukujuza kuwa maganda hayo ya viazi mviringo yanapotumika vyema huweza kuwa tiba ya tatizo la baridi yabisi kwa lugha ya kingereza ugonjwa huu huitwa ‘Arthritis’ .

Mtu mwenye ugonjwa huu hupata maumivu makali ndani ya misuri na maungio mbalimbali ya mwili.

Tatizo hili la baridi yabisi linapokosa kutibiwa mapema huweza kusababisha ulemavu kwa mgonjwa na mbaya zaidi ugonjwa huu huweza kumkuta mtu yeyote pasipo kujali umri au jinsia.

Viazi mviringo na maganda yake
 Kuna wakati miili yetu kutokana na sababu Fulani Fulani utumbo mkubwa hushindwa kunyonya chumvi za muhimu kutoka katika mzunguko wa damu.

Upungufu wa chumvi iitwayo soda fosfeti (phosphate of soda) ndani ya chembechembe za mwili huweza kusababisha ugonjwa wa baridi yabisi.

Lakini pale tunaposema maganda ya viazi mviringo huweza kusaidia kuondokana na tatizo hili ni pale ambapo yatatumika kam ifuatavyo;

Chukua kilo moja ya maganda ya viazi mviringo, yaoshe vizuri, ongeza maji lita moja na nusu kisha chemsha kwa muda wa dakika 20.

Baada ya kufanya hivyo chuja maji hayo na uyatunze mahali safi na salama na utakuwa ukitumia maji hayo kiasi cha glasi moja mara nne kwa muda wa siku ishirini na moja, lakini ni vyema ukawasiliana nasi zaidi kama unasumbuliwa na tatizo hili kwa muda mrefu kwa mawasiliano yafuatayo ; 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300 Barua pepe, dkmandaitz@gmai

No comments:

Post a Comment