Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 15 May 2015

JE, UNAZIFAHAMU SABABU ZA MWANAMKE KUSHINDWA KUSHIKA MIMBA? MAJIBU YAPO HAPA


Tatizo la kushindwa kushika mimba ni moja la tatizo ambalo huwasumbua watu wengi katika jamii tunazoishi. Kitaalam tatizo hili huitwa infertility.


Kimsingi watu wengi hutarajia kupata mtoto endapo wanadoa watakuwa wakishiriki tendo la ndoa pasipo kutumia kinga ndani ya miezi mitatu.

Hata hivyo, kuna baadhi ya wanandoa hushiriki tendo hilo kwa kipindi chote hicho pasipo kutumia kinga lakini bado huwa ni mtihani kwao kwa mama kushika mimba, sasa napenda kukuapa hizi sababu ambazo huweza kuchangia tatizo hilo.

Kuna sababu nyingi za tatizo hili, lakini baadhi yake ni hizi zifuatazo:

Tatizo hili huweza kuchangiwa na kutopevuka kwa mayai kwa mwanamke, ambapo mwanamke anapata siku zake kama kawaida, lakini hapevushi mayai

Baadhi ya wanawake pia huweza kujikuta katika tatizo hili kutokana na kuwa na matatizo ya homoni. hii huweza kuchangiwa kutokana na matumizi ya baadhi ya vyakula au vipodozi fulani fulani.

Shida nyingine ambayo huweza kuchangia tatizo hili ni kutokea kwa hitilafu katika mirija ya uzazi ikiwa ni pamoja na kupata maambukizi katika via vya uzazi.

Lishe duni nayo ni moja ya sababu inayoweza kuchangia mwanamke ashindwe kushika ujauzito

Pamoja na hayo, sababu nyingine ni matatizo ya mbegu za kiume (Sperm disorders). Kutokuwa na ubora wa kutosha wa kutungisha mimba.

Pindi unapoona umekaa muda mrefu bila kupata ujauzito na umekuwa ukishiriki tendo la ndoa bila kinga yoyote kwa zaidi ya miezi mitatu mine na kuendelea basi ni vyema ukawaona madaktari kwaajili ya uchunguzi wa kina zaidi ili kubaini tatizo lako.

Pia unaweza kufika kwetu Mandai Herbal Clinic na utafanyiwa uchunguzi kisha utapewa dawa ambazo zitakusaidia kuondokana na tatizo hilo. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au tupigie simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment