Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 11 May 2015

JE, UNAZIJUA FAIDA ZA KUFANYA MAZOEZI YA KUKIMBIA? ZIPO HAPAWakati tatizo la unene likizidi kuongezeka katika jamii yetu, watu bado wamekuwa wakijisahau kufanya mazoezi.

Kimsingi binadamu yoyote mwenye maarifa ya namna ya kula vizuri na kufanya mazoezi kwa afya, huwa na upeo mzuri na mkubwa wa kujua na kuelewa mambo.


Kukimbia ni moja ya zoezi ambalo lina manufaa mengi, hizi hapa ni baadhi ya faida zake

Husaidia kuimarisha moyo na mapafu
Kwa mtu wa kawaida mwili hutumia oxygen mara 10 zaidi wakati wa kufanya zoezi rahisi la kukimbia ukilinganisha na akiwa amekaa. Mtu anapofanya zoezi la kupasha mwili kwa muda huimarisha mfumo wa moyo wa usukumaji damu na hivyo husaidia moyo na mapafu kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.

Huimarisha utendaji kazi wa ubongo na kuongeza uwezo wa kufikiri
Inaaminika mazoezi ya kukimbia husababisha ubongo kuzalisha homorne iitwayo ‘’endorphin’’ ambayo kemikali hii huibua hisia za furaha na kumfanya mtu kuwa katika hali ya kuwa na raha na mwenye mawazo chanya.

Sio tu kwamba mazoezi haya yatakufanya ujihisi katika hali ya furaha kwa muda bali yatakufanya pia uongeze ujasiri wako wa kujiamini na kujikubali mwenyewe na hivyo pia utapunguza msongo wa mawazo na matatizo mengine yanayosababishwa na kuchoka kwa ubongo.

Hupunguza uzito wa mwili na mafuta mwilini
Sote tunajua unapofanya mazoezi, baada ya muda utajisikia kuchoka, kutokwa na jasho, kuhema sana nakadhalika.

Hayo yote ni matokeo baada ya kufanya zoezi la kukimbia, unapofanya zoezi la kukimbia unachoma calories mwilini na hatimaye kupunguza mafuta. Ikiwa utakuwa unafanya mazoezi ya kukimbia ipasavyo na kwa malengo ni rahisi kwako kuona mabadiliko ya mwili wako baada ya wiki chache.

Ikiwa wewe ni mnene na una uzito mkubwa wa mwili huu ndio wakati wako wa kuanza kufanya mazoezi ya kukimbia, lakini kama una matatizo yoyote ya kiafya ni vyema ukamuona daktari kwa ushauri kabla ya kuanza kufanya mazoezi haya.

Mandai Herbal Clinic inaendelea kukukumbusha kwamba endapo unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo yale sugu unaweza kufika kituoni kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata suluhisho la matatizo yako. Pia unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.    

No comments:

Post a Comment