Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Thursday, 14 May 2015

JE, UNGEPENDA KUFAHAMU MALENGO YA MILENIA KATIKA SEKTA YA AFYA YAMEFIKIA WAPI ? MAJIBU YOTE YAPO HAPA


Ikiwa mwaka huu wa 2015 ndio mwaka wa ukomo wa malengo ya maendeleo ya milenia yaliyoafikiwa na viongozi wa serikali mwaka 2000 ikiwa ni mbinu ya na muongozo wa juhudi za kutokomeza umasikini.


Kwa mujibu wa takwimu za afya duniani zilizotolewa hapo jana na Shirika la Afya Duniani (WHO) zimetathimini kuwa hatua zilizopigwa katika malengo hayo ya milenia ya afya kwa nchi 194 matokeo yameonesha ni mchanganyiko.

Aidha, ripoti hiyo imebainisha kuwa ifikapo mwisho wa mwaka huu dunia itakuwa imetimiza malengo ya kukabiliana na maradhi kama ukimwi, malaria na kifua kikuu na kuongeza upatikanaji wa maji salama ya kunywa.

Mbali na hayo, ripoti hiyo imesema kuwa, hadi mwisho wa mwaka huu kutakuwa kumepigwa kwa hatua kubwa katika kupunguza utapia mlo kwa watoto, vifo vya kina mama na watoto wachanga na kuboresha hali ya usafi.

Naye Dr. Ties Boermat ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Takwimu za afya wa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) anasema kuwa "bila shaka takwimu hizi zinazingatia malengo ya maendeleo ya milenia, hizi si takwimu za mwisho mwisho sababu mwaka bado haujaisha, lakini ni makadirio mazuri na thabiti na yanatupa taswira ya hali halisi ilivyo duniani katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya milenia, kumekuwa na maendeleo mazuri na yenye kutia moyo katika kipindi cha miaka 25 , hasa katika mapambano dhidi ya ukimwi, kifua kikuu na malaria.

Asante kwa kuendelea kuwa karibu nasi, tunapenda kukukaribisha pia kutangaza nasi biashara yako kupitia tovuti yetu hii. Tupigie simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment