Wednesday, 20 May 2015

JENGA UTAMADUNI WA KUTUMIA BAMIA UPATE FAIDA HIZIBamia ni miongoni mwa mboga za majani ambazo kwa kawaida hulimwa zaidi kwenye maeneo yenye joto, ukanda wa kitropiki ikiwamo mikoa ya Singida na Dodoma.Pia bamia inafahamika kwa wengi katika jamii kwa ladha yake nzuri inapotumika kama mboga katika baadhi ya milo.

Zifuatazo ni baadhi ya faida za kutumia bamia kiafya:
Bamia ina wingi wa vitamini A ambayo husaidia kuupa mwili kinga ya kupigana na maradhi, lakini kwa wale wenye matatizo ya kuona, kula bamia mara kwa mara husaidia kuimarisha mwanga katika macho yako.

Pia bamia zina wingi wa vitamini K ambayo husaidia kuimarisha mifupa na kuganda kwa damu.

Mbali na hayo, uteute unaopatikana kwenye bamia husaidia kuunda tishu za mwili na ngozi. Hivyo kusaidia husaidia kujenga ngozi.

Ikiwa ungependa kufika Mandai Herbalist Clinic na kufahamu mengi zaidi kuhusu mimea tiba, mitishamba, nafaka  na matunda ni vyema ufanye mawasiliano nasi kupitia 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Namba zetu hizo pia zinapatikana kwenye whatsapp. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam  

No comments:

Post a Comment