Tuesday, 5 May 2015

JITIBU MAUMIVU YA TUMBO
Mara nyingi tumekuwa tukisikia baadhi ya watu wetu wa karibu au sisi wenyewe tukilalamika kusumbuliwa na tumbo lisilo la vidonda wala ugonjwa wowote ila utasikia mtu anakwambia tumbo linanikata, huenda akawa anavurugikwa na tumbo.


Unapokunywa  maziwa mtindi huweza kusaidia sana tumbo lako hasa pale linapokuwa kwenye hali ya kuvurugika kurejea katika hali nzuri.

Hakikisha unapotumia maziwa hayo epuka yenye sukari nyingi ikiwezekana jaribu kunywa bila sukari pia.

Aidha, kinywaji hiki kina tibu mambo mengi kwani mbali na tumbo pia husaidia kutibu msongo wa mawazo na kuweka sawa akili.

Mbali na kutumia maziwa mtindi pia unaweza kuchukua tangawizi kisha isage halafu kamua maji yake kisha weka kwenye kinywaji chochote chaweza kuwa cha baridi au cha moto ni dawa pia.

Pamoja na hayo, ni vyema kuwaona wataalam wa afya zaidi endapo utaona hali ya maumivu imekuwa ikiongezeka zaidi ili uweze kuchunguzwa na kujua nini chanzo cha maumivu hayo zaidi. 

Pia unaweza kufika Mandai Herbal Clinic na kuonana nasi ili tuweza kuona namna ya kukusaidia kliniki yetu ipo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana nasi kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. No comments:

Post a Comment