Wednesday, 27 May 2015

JOTO KALI NCHINI INDIA LIMEENDELEA KUSABABISHA WATU KUFARIKI NA SASA WAMEFIKIA WATU 800


Kufuatia hali ya joto kupanda kwa kasi kubwa nchini India mwezi uliopita, hali hiyo imesababisha watu 800 kupoteza maisha yao.

Joto hilo limeonekana kuathiri zaidi katika maeneo ya majimbo ya Andhra Pradesh na Telangana yanayopatikana kusini mwa nchi hiyo kwa nyuzi joto 48,, huku watu wengi waliofariki wakiwa ni wafanyakazi wa ujenzi au wasio na makazi.

Aidha, madaktari wamesema kuwa ukosefu wa maji mwilini na kuchomwa na jua kali ndio sababu zilizopelekea idadi kubwa ya watu kupoteza maisha walipokuwa hospitalini.

Pia hali hiyo ya joto kali haijawaathiri binadamu tu bali na wanyama pia.

Wakati hayo yakiendelea nao watabiri wa hali ya hewa ,wametoa taarifa ya kunyesha kwa mvua siku chache zijazo, ingawa hali hiyo ya joto inatarajia kuendelea kwa muda wa wiki mbili.

Maafisa wa umma, wamewahimiza wananchi kuyahama makazi yao mapema iwezekanavyo na kuwashauri kunywa maji mengi.

Chanzo:TRT - Swahili

No comments:

Post a Comment