Friday, 22 May 2015

JUISI ZA MATUNDA NI MUHIMU SANA KWA AFYA LEO TUNAANZA NA HII YA NANASINanasi ni moja ya tunda ambalo hupendwa na watu wengi ulimwenguni si kwasababu ya kutambua faida zake, lakini ni kutokana na kuwa na ladha nzuri pia.

Matumizi ya juisi halisi ya nanasi huenda yakawa na faida pia katika miili yatu kutokana na kuwa na virutubisho kadhaa ambavyo ni muhimu mwilini pia.

Miongoni mwa faida za kunywa juisi halisi ya nanasi ni pamoja na kusaidia mmen’genyo wa chakula kuwa katika hali nzuri zaidi.

Kunywa juisi ya nanasi pia huasidia sana kuimarisha mifupa ya mwili, kutokana na juisi hiyo kuwa na madini ya ‘manganese’. Kimsingi glasi moja ya juisi ya nanasi ni sawa na kupata asilimia 73 ya madini hayo ya manganese. Hivyo nanasi husaidia ukuaji wa mifupa kwa watoto wadogo pamoja na kuimarisha mifupa wakati wa umri mkubwa (uzeeni).

Pia unywaji wa juisi ya nanasi husaidia sana kuongeza kinga ya mwili pamoja na kuboresha afya ya ngozi, huku ikisaidia pia katika kumpatia mhusika uwezo mzuri wa kuona na hii ni kutokana na kuwa na vitamin A ndaini yake. Hivyo matumizi ya mara kwa mara ya juisi ya nanasi yataweza kukusaidia kuepuka matatizo ya kuwa na uoni hafifu hapo baadaye katika umri mkubwa.

Kunywa juisi hii ya nanasi pia kutasaidia sana kukuondolea tatizo la kuhusi maumivu ya viungo ‘arthritis’. Juisi ya nanasi husaidia sana kupunguza maumivu ya viungo kwa watu wazima (wazee) ambao mara nyingi wamekuwa wakisumbuliwa na matatizo hayo.

Ukweli ni kwamba juisi ya nanasi imebarikiwa kwa kusheheni madini na vitamin nyingi za kutosha sana. Kuhusu vitamin juisi hii ina vitamin C, B Complex, na imebarikiwa pia kuwa na madini ya 'potassium', 'calcium', 'manganese' na 'phosphorous', huku ikiwa na utajiri mkubwa wa 'fiber' yaanu nyuzinyuzi ambazo huwa na umuhimu pia na kukinga dhidi ya tatizo la kukosa choo ‘consumption.’

Juisi halisi kabisa ya nanasi huwa na asilimia 75 ya kiwango cha vitamin C , huku vitamin hiyo ikiwa ni muhimu sana katika mfumo wa kinga mwilini.

Nanasi pia linauwezo wa kukuepusha na matatizo ya shinikizo la damu yaani high blood pressure, kwahiyo inashauriwa mtu mwenye tatizo hilo kujenga utamaduni wa kutumia juisi ya nanasi mara kwa mara.

Kimsingi kuna mengi ya kuzungumza kuhusu faida za juisi hii, lakini kwa ufupi ni kwamba faida nyingine za juisi hii ni kulinda afya ya meno na moyo pamoja na kuwasaidia wale wenye kuhitaji kupunguza uzito


Anza sasa kutangaza nasi kupitia tovuti hii kwa gharama nafuu sana tupigie kwa simu namba; 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment