Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 18 May 2015

KARANGA NAZO ZINA UMUHIMU WAKE KATIKA KUBORESHA AFYA YAKO


Tunapozungumzia kuishi vizuri ni pamoja na kula chakula bora na sahihi. Pia, mtu anayeishi vizuri ni yule ambaye hasumbuliwi na maradhi mara kwa mara hata kama hana kipato kikubwa.

Karanga ni moja ya vyakula ambavyo huwekwa katika orodha ya vyakula ambavyo huweza kumsaidia mtu kuwa na afya nzuri kwa yule ambaye alikuwa hana afya bora na yule ambaye alikuwa tayari ana afya nzuri na bora basi ataendelea kuwa na afya nzuri zaidi.

Unaweza ukazidharau karanga, lakini zina faida kubwa mwilini. Miongoni mwa faida zake ni pamoja na kuimarisha afya ya moyo, hupunguza kolestro mbaya mwilini na kuongeza kolestro nzuri.

Mafuta mazuri yaliyomo kwenye karanga hupunguza shinikizo la juu la damu na huponya magonjwa ya moyo na hupunguza uzito.

Faida zote hizi unaweza kuzipata kutoka kwenye karanga au siagi iliyotengenezwa kutokana na karanga (peanut butter). Ni vizuri ukala kiasi fulani cha karanga kila siku, hasa za kuchemsha ndiyo nzuri.

Ikiwa ungependa kufika Mandai Herbalist Clinic na kufahamu mengi zaidi kuhusu mimea tiba, mitishamba, nafaka  na matunda ni vyema ufanye mawasiliano nasi kupitia 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment