Tuesday, 26 May 2015

KIFO CHA KIONGOZI WA UPINZANI CHA SABABISHA KUREJEA KWA MAANDAMANO ZAIDI BURUNDI
Maandamano nchini Burundi yamerejea tena kufuatia kuuawa kwa kiongozi wa chama cha upinzani, Zedi Feruzi .

Katika maandamano hayo waandamanaji wamekuwa wakichoma moto magari ikiwa ni pamoja na basi moja la uchukuzi ambalo lilichomwa moto mjini Bujumbura Burundi.

Waandamanaji hao wamerejea barabarani ili kupinga uamuzi wa Rais Pierre Nkurunzinza kuwania muhula waa tatu.


Nao wanaharakati wa upinzani nchini humo wamesitisha mazungumzo na serikali ya Rais Pierre Nkurunziza ya kutaka kutanzua mzozo ulioko wa kisiasa.

Kufuatia machafuko hayo tayari zaidi ya raia 100,000 wa taifa hilo wametorokea mataifa mengine ya jirani.

No comments:

Post a Comment