Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 7 May 2015

KIPANDE CHA PAPAI NI SULUHISHO TOSHA LA TATIZO LA NGOZI YAKO


Papai ni moja ya tunda ambalo si geni miongoni mwa watu wengi hapa nchini na wengi wetu tunda hili limekuwa katika orodha ya matunda ambayo tunatumia na huenda tunalipenda pia.
Inawezekana wewe unalipenda tunda hili kutokana na ladha yake nzuri, lakini leo nataka uzidi kulipenda zaidi tunda hili kutokana na huu uwezo wake mwingine wa kutunza ngozi yako.

Papai ni moja ya tunda ambalo linapotumika vizuri huweza kuwa msaada katika kuweka ngozi yako katika hali nzuri hususani masula ya kuondosha mikunjo katika ngozi.

Ili tunda hili likusaidie kutunza ngozi yako unachopaswa kufanya ni kuchukua kipande kimoja cha papai, kisha changanya na unga wa ngano kijiko kimoja halafu tumia mchanganyiko huo kwa kuupaka ile sehemu iliyoathirika (yenye mikunjo). Kisha uache mchanganyiko huo mwilini mwako kwa muda wa dakika zisizopungua kumi halafu nawa vizuri kwa maji safi na salama.

Fanya zoezi hilo mara kwa mara angalau mara moja kwa siku ikiwezekana usiku kabla ya kulala na baada ya siku kadhaa basi utaanza kuona mabadiliko katiko ngozi yako.

Pia inapobidi ni vizuri kupenda kulila tunda hili la papai kutokana na kuwa na virutubisho vingi muhimu ikiwemo vitamin A, B, C, D pamoja na E.

Tunapenda kuendelea kukukaribisha Mandai Herbal Clinic, endapo unasumbuliwa na matatizo mbalimbali ya kiafya, tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Au wasiliana nasi kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment