Monday, 11 May 2015

KUNA HIZI SIFA ZA MDALASINI KATIKA TIBA


Mdalasini ni moja ya kiungo kizuri ambacho hutumika kuongeza ladha nzuri katika kinywaji.

Mdalasini unaweza kutumika kuanzia magome, na mafuta yatokanayo na magome na kwenye majani.

Unapotumia unga wa magome yake huweza kutibu magonjwa mbalimbali yakiwemo matatizo ya ugumba ambapo mwanaume anapaswa kutumia vijiko viwili vya mdalisini pamoja na kuchanganya na asali katika mlo wa jioni.

Kwa kutumia mchanganyiko huo huo pia husaidia wanawake kuhamasisha kizazi.

Aidha, mchanganyiko huo wa asali na mdalasini husaidia kuondosha lehemu (cholesterol) mwilini

Pia mdalasini na asali husaidia kutibu mafua pamoja na kikohozi

Mbali na hayo, pia mdalasini husaidia kuzuia na kuondoa gesi tumboni, vidonda vya tumbo, kichefu chefu na kutapika, kuharisha , kutia joto tumbo lililopoa.

Hayo ni baadhi ya manufaa ya mdalasini endelea kuwa karibu nasi ili kupata elimu ya mimea tiba na masuala ya afya kwa ujumla kwa kulike page yetu ya facebook iitwayo Mandai Herbalist Clinic -mhc

Unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment