Wednesday, 20 May 2015

KUNYWA MAJI NI MUHIMU SANA TUSIPUUZE!


Kunywa maji safi na salama kwa kiasi kinachostahili kiafya kunaweza kuboresha maisha yako na kumfanya mtu kujihisi mwenye afya na furaha zaidi.


Kunywa maji ya kutosha kuna faida nyingi miongoni mwa faida hizo ni kama zifuatzo;

Maji husaidia mmeng'enyo wa chakula. Pia maji yanahusika katika kulainisha baadhi ya vyakula, huku maji ya kutosha huongeza ufanisi wa mwili katika kusharabu chakula.

Maji husaidia kuboresha afya ya ngozi. Kunywa maji ya kutosha hupendezesha ngozi na kuipa muonekano mzuri pamoja na kusaidia kuboresha tishu za ngozi na kuongeza unyevu kwenye ngozi.

Faida nyingine ya maji ni kusaidia katika utendaji wa ubongo. Maji yanauweka ubongo katika hali nzuri zaidi na ya ufanisi zaidi. Hivyo kunywa maji ya kutosha humuwezesha mtu kufikiria vyema zaidi.

Faida nyingine za maji ni kusaidia kuepuka baadhi ya magonjwa. Mfano mafua, mawe ya figo, matatizo ya ini.

Maji pia husaidia kwa wale wenye matatizo ya kupata choo kikavu. Kunywa maji ya kutosha kunaweza kukusaidia kupata haja kubwa kiulaini na hivyo kukepusha na tatizo la constipation au kuwa na choo kigumu.

Kunywa maji ya kutosha husaidia kupunguza tatizo la kubanwa na misuli na pia hupunguza msuguano katika viungo vyako.

Kama upo katika mkakati wa kupunguza uzito ni vyema ukatumia pia maji kwani husaidia sana kupunguza uzito.

Ikiwa ungependa kufika Mandai Herbalist Clinic na kufahamu mengi zaidi kuhusu mimea tiba, mitishamba, nafaka  na matunda ni vyema ufanye mawasiliano nasi kupitia 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Namba zetu hizo pia zinapatikana kwenye whatsapp. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment